Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MTAKWIMU kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mdoka Omary amesema mwishoni mwa mwaka huu watakuwa na ripoti inayohusu utafiti wa watu wanaoweza kufanya kazi, ambapo mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014.
Aidha, amesema wametoka kumaliza kukusanya taarifa hizo mwezi Juni,2021, wanategemea kutoa taarifa hizo kulingana na ratiba ya machapisho itakavyokuwa inaruhusu.
Mtakwimu Omary, alisema jana wakati akiwa katika banda la NBS katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam, ambapo wananchi wengi walitaka kujua jinsi taarifa zinavyokusanywa.
Alisema, huwa wanatakwimu zingine ambazo wanafanya au tafiti, ambapo utafiti zinafanyiaka kila baada ya miaka mitano ikiwemo utafiti ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.
Omary alisema jukumu lingine ambao ofisi ya inafanya ni kuratibu zoezi la sensa ya watu na makazi, tangu Uhuru wameshafanya sensa tano na ya mwisho ilikuwa 2012, na kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kufanya sensa ya makazi 2022.
"Nawaomba wananchi watoe ushirikiano kwa karani wa sensa atakapo kwenda kutembelea Kaya na kuuliza maswali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuweza kupata taarifa mbalimbali yanayolenga sensa hiyo,"alisema Omary
Akizungunzia nyenzo ambazo zitatumika wakati wa ukusanyaji wa taarifa za sensa watu na makazi watakuwa na madodoso yasiyopungua mawili, watakuwa na dodoso Kuu na dodoso la jamii ambao litakusanya taarifa za kijamii katika eneo la kuhesabia watu.
Pia, watakuwa na dodoso moja kwa ajili ya watu wasio na makazi maalum ambao ni wasafiri, pamoja na wagonjwa waliyolazwa hospitalini.
" Hayo ndiyo madodoso ambayo yatatumika, lakini pia tutakuwa na maswali mengi kulingana na taarifa ambazo sisi tunazihitaji ambapo tutakuwa na masuala ya demokrasi yanayohusu umri, jinsia, masuala ya ulemavu, hali ya uchumi pamoja na masuala ya hali ya makazi,"
"Tu nataka kujua nyumba zao zimeezekwa na nini na pia zimesakafiwa na kitu gani na pia masuala ya uhamaji," alisema Omary
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment