EWURA yaja na uwekezaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu. | Tarimo Blog


 
Meneja Uhusiano na  Mawasiliano kwa Umma wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo akizungumza kuhusiana na soko la mafuta katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 
 
*Ni katika urahishaji wa upatikanaji wa nishati ya mafuta
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa imetengeneza  mazingira ya ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini vitakavyotumia  gharama nafuu.

Kuwepo kwa utaratibu huo ni mahitaji ya mafuta Petroli na Dezeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka kutokana na kushamiri kwa shughuli za uchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Akizungumza na Michuzi TV Meneja Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Titus Kaguo katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa maeneo ya vijijni hayana vituo vya mafuta kutokana na wawekezaji wa biashara hiyo kusita kuweka mitaji kujenga vituo vya kuuzia mafuta kwa kuona maeneo hayo hakuna biashara ya kutosha.

Kaguo amesema kuwa licha wafanyabiashara wa  mafuta ya Petroli na Dizeli kusita kuwekeza kimefanya wafanyabiashara biashara wenye mitaji kidogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta  wameingia kufanya biashara hiyo kwa kutumia miundombinu haafifu na isiyo salama kama vile kuhifadhi mafuta kwenye madumu ya plastiki ,mapipa na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

Amesema mahitaji na mambo kuzingatia wakati Ujenzi kituo cha mafuta kijijini kwa wenye mitaji kidogo ni Kiwanja kilichopimwa na Mamlaka husika Halmashauri ya Kijiji imeridhia kwa  kitumike katika biashara ya kituo cha mafuta na kiwanja hicho ili kikidhi viwango vilivyowekwa kinatakiwa kuwa na ukubwa was mita za mraba 400

Hata hivyo amesema angalau kwa biashara ya mafuta maeneo ya vijijni angalau anaanza na tenki moja ya kuhifadhia mafuta na kama atauza aina moja anatakiwa kuongeza sawia na kuwa na ujazo angalau lita 4500 Au 5000 na kuwa na pampu ya Mkono mmoja au mwili kulingana na aina za mafuta.

Amesema mambo mengine ni katika  ujenzi no bomba nne za chuma za inchi nne na urefu mita tank kwa ajili ya kujengea paa na uhitaji wa bomba za inchi moja na nusu na bati kwa ajili ya kenji na kuezeka na masuala mengine ya uhifadhi wa mafuta hayo.

Amesema baada EWURA kubaini kuwepo kwa biashara ya mafuta ya kiholela na salama maeneo ya kijijini imekuja kanuni za Ujenzi wa vituo mafuta katika maeneo hayo ikiwa kwa mtu yeyote anayetaka kujenga kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate  kibali cha mamlaka hiyo, baada ya kutuma maombi, pia baada kuanza biashara hiyo.
 
Amesema mwekezaji katika maeneo ya vijijni kwa ajili ya biashara ya mafuta ya Petroli na Dizeli  anatakiwa kuwa na leseni ya EWURA ambayo hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote na kugagua kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.
Kutengeneza kwa mazingira ya ujenzi
 
 
 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2