KAMPUNI ya Tecno mobile Tanzania imezindua simu mpya ya kisasa aina ya tecno Phantom X yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zozote.
Simu hiyo yenye ukubwa wa GB 256 itamsaidia mtumiaji kuhifadhi data zake kwa urahisi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa simu kujaa.
Meneja masoko wa Tecno Mobile Tanzania William Mota amesema simu hiyo ina Ram 8 ambayo inawezesha kufanya kazi kwa haraka zaidi na ni nzuri kwa matumizi mbalimbali katika kuhifadhi kazi zao pamoja na ukubwa wa kioo chake no Inch 6.7 kioo ambacho kitawasaidia wale wote wanaopenda kusoma kupitia simu kwa usahihi.
Aidha Mota amewatoa hofu watumiaji wa simu hiyo kwa kueleza kuwa simu hiyo itakidhi mahitaji yao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment