KELELE NA MITETEMO NI UCHAFUZI WA MAZINGIRA Dkt. GWAMAKA | Tarimo Blog

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka, akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani), Juu ya suala la kelele na mitetemo kwenye Baa na Kumbi za starehe katika ofisi za NEMC Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini taarifa zinazotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka (hayupo pichani).



MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka, amesema kuwa kelele na mitetemo ni moja wapo ya uchafuzi wa mazingira hasa pale inapozidi viwango na inapelekea madhara kwa viumbe hai na binadamu.


Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa NEMC Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kelele zinazozidi viwango katika Baa, Kumbi za starehe hata katika nyumba za ibada zinasababisha athari kubwa sana katika jamii yetu na kupelekea malalamiko kwa wakazi wanaokaa maeneo hayo. 


Aidha Dkt. Gwamaka amewataka wanaomiliki Baa, nyumba za starehe pamoja na nyumba za Ibada kuweka kipimia sauti (sound proof), ili kuzui kelele hizo kutoka nje na kutosumbua watu wengine. Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni ya mazingira 2005 ambayo imeainisha viwango vya kelele maeneo ya makazi, biashara, viwanda na maeneo ya huduma za kijamii.


“Tutambue kuwa kelele inapozidi viwango uathiri afya ya mwanadamu na wanaoathirika sana ni watoto na wazee. Inapaswa kujua kuwa pale unapopiga kelele kupita kiasi inapunguza umakini, kupelelea migogoro, kupelekea vifo, kupata ukiziwi, msongo wa mawazo kutokana na kukosa utulivu, kutokulala, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kupelekea shinikizo la damu, hivyo hizi kanuni zimewekwa ili kulinda afya za binadamu na kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa ujumla.”Dkt. Gwamaka


Ameendelea kusema kuwa kila binadamu anahaki ya kuishi hivyo kutokana na Serikali kujali Wananchi wake ndio maana Kanuni na Sheria ya kudhibiti kelele ikawekwa. Dkt Gwamaka amewataka wananchi kufata sheria bila shuruti hivyo Baa, Kumbi za starehe na nyumba za ibada zizingatie viwango vilivyowekwa ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi wengine.


Dkt Gwamaka amesema katika kuhakikisha tunalinda afya ya jamii Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji, wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia, Wizara ya Mambo ya Ndani kwa pamoja Mawaziri walikaa baada ya kuona hizi kelele zimepitiliza viwango na wametoa maelekezo kuwa kila mwananchi afanye shughuli zake bila ya kusababisha kelele na mitetemo iliyozidi viwango.


“Mawaziri saba wamekaa kujadili hili nikiwa kama Mkurugenzi Mkuu nitatekeleza maagizo yao, hivyo naomba kila mtu afuate sheria na kwa mwananchi yoyote atakapoona kumbi za starehe, Baa au nyumba za Ibada zinapiga kelele naomba mtoe taarifa kupitia namba 0800110115/0800110117/0800110116 bure. Onyo kwenye hili hatutatania fuata sheria ya Nch. Dkt. Gwamaka



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2