Mbolea ya Hakika iliyokuwa packed kwenye mifuko kwa ajili ya kutumiwa na wakulima.
Bango lenye kuonyesha ubora wa mbolea hiyo shambani kwenye zao la parachichi.
Baadhi ya wakulima,viongozi na washiri wa hafla hiyo ya uzinduzi wakiwa katika zoezi la uzinduzi wa mbolea lillofanyika mjini Njombe na kuwapa fursa wakulima kunza kuitumia rasmi mbolea hiyo.
Na Amiri Kilagalila,Njombe
SERIKALI mkoani Njombe imezindua mbolea ya asili "Hakika" inayofanya vizuri kwenye kilimo cha parachichi huku wakulima mkoani humo wakihamasishwa kutumia mbolea hiyo kutokana na wananchi wengi mkoani Njombe kulima kwa kiasi kikubwa tunda la Parachchi hivi sasa.
Ili kuboresha kilimo cha zao la parachichi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Guavay ya Jijini Dar es salaam wamekuja na ubunifu wa kutumia mabaki ya mimea mbalimbali na kuzalisha mbolea mpya ya Asili inayofahamika kwa jina la HAKIKA lengo likiwa ni kuongeza tija na ubora wa zao hilo.
Mratibu wa mradi wa mbolea ya Hakika kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Professor Amelia Kivaisi amesema katika utafiti uliofanywa umebaini kuwa mbolea ya Hakika inasifa ya kuongeza tija ya ukuzaji wa mimea na kurutubisha udongo ulioharibiwa na kemikali.
"Kwetu sisi chuo kikuu cha Dar es Salaam hii ni siku muhimu sana na tunatambua kuwa nchi yetu ya Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi,zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wote wanajishughulisha na kilimo na wanaishi maeneo ya vijijini"alisema Prof,Amelia Kivaisi
Naye mratibu wa mradi na mhandisi Ahad Katera ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Guavay amesema "Hadi sasa tayari tumekwishawekeza zaidi ya Bilioni 1.5 katika miundombinu tafiti za masoko malighafi,teknolojia za kuongeza uzalishaji pamoja na mashamba darasa"
Akiongea kwa niaba ya wakulima wa Parachichi mkoani Njombe, mmoja wa mashuhuda wa Matumizi ya Mbolea hiyo Erasto Ngole amekiri kuwa katika Mkoa wa Njombe iwapo wakulima watapewa elimu kutoka kwa maafisa ugani watanufaika na matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo zenye kuleta tija shambani, kauli iliyoungwa mkono na Mbunge wa Njombe Mjini Mheshimiwa Deo Mwanyika.
"Matokeo yalikuwa ni ya kuridhisha,na mbolea ilifanya kazi nzuri sana tangu waliponza kufanyia utafiti shambani kwangu mwaka 2017 na nilipata matokeo makubwa kwa kuvuna matunda makubwa,mazuri yasiyo na mabaka"alisema Erasto Ngole Mkulima wa Parachichi
Naye mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika alisema "tunataka tupate bei nzuri ya parachichi zetu na moja ya mambo ambayo kampuni hii ya leo ambayo imezindua Mbolea na imetuhakikishia kuwa mbolea hii imepata uthibitisho"
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mbolea hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi.Kissa Kasongwa ameipongeza Kampuni ya Guavay kuja na mbinu mpya ya kuwa na mbolea ya Hakika na kwamba ndani ya wilaya ya Njombe ambapo mwitikio wa wakulima wa zao la Parachichi ni mkubwa utaenda kuwanyanyua wakulima.
"Na nitoe wito kwa maafisa ugani wote kuhakikisha wanawatembelea wananchi na kuwaeleza vitu muhimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia afya ya udongo "alisema Kissa Gwakisa Kasongwa
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment