*Wataalamu wa Ugavi na manunuzi waaswa kushiriki mafunzo hayo mhimu
* Zaidi ya wataalamu 150 wameshapata mafunzo
CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar Es Salaam wakishirikiana na Kuehne Foundation watoa mafunzo ya manunuzi ya vifaa tiba na mitambo ya hospitali kwa wataalamu wa Ugavi na Manunuzi kutoka taasisi za Umma na Taasisi Binafsi.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo leo Julai 16,2021 Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Mshauri na Mkurugenzi wa Medal Investiment, Christopher Msemo amesema kuwa wataalamu wa famasia sio wataalamu wa manunuzi hivyo nivyema kushirikiana wafamasia na wataalamu wa manunuzi kununua dawa na vifaa tiba vinavyohitajika katika taasisi.
"Vifaa tiba na mitambo ya hospitali inachukua sehemu kubwa ya kasma ya taasisi husika na watu wanaotegemewa zaidi ni wataalamu wa Ugavi na manunuzi kwani wao sio madaktari, sio wauguzi na sio Mafamasi lakini kulingana na taaluma yao ya ugavi na utunzaji ndio wanahiyo dhamana." Amesema Msemo
Licha ya hayo Msemo amesema kuwa mafunzo hayo yanatoa mwongozo wa kuepukana na matatizo makubwa yanayojitokeza katika taasisi za afya katika manunuzi ya vifaa tiba na mitambo hospitalini. "Hata hivyo mafunzo hayo yanawatahadharisha wataalamu wa Ugavi na manunuzi kuwa sio vifaa na mitambo yenye bei rahasi kuwa ndio salama kwa serikali au kwa taasisi."
"Unaweza kupewa mtambo bure na ukafanya kazi lakini ukashindwa kuuendeleza ule mtambo kwa sababu ya kutegemea vitendanishi, vipuli au taaluma ya kutengeneza mtambo huo hivyo lazima utegemee wataalamu kutoka kule ulikopewa mtambo... kwahiyo matokeo yake inakuwa gharama kubwa kuliko hata ungenunua mtambo mpya na kwa gharama kubwa. Ametoa mfano Msemo.
Hata hivyo Msemo amesema kuwa ni bora kutumia wataalamu wa manunuzi na ugavi hapa nchini kuliko kupewa msaada wa vifaa tiba na mitambo bila kuwa na utaalamu wa vifaa hivyo. Unaponunua vifaa kama hivyo usiangalie bei angalia ile taarifa za kitu unachokinunua na wataalamu wa kutumia pamoja na namna y kutengeneza na sio kutegemea mtaalamu kutoka nje ya nchi.
Kwa Upande wake Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu na Mzumbe na Mratibu wa Mradi wa Kuehne Foundation Daktari Omary Swalehe amesema kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya tatu kwa watalaamu wa ugavi na manunuzi katika sekta ya afya na jumla ya wataalamu 150 wameshapata mafunzo hayo.
Hata hivyo Dkt. Omary amesema kuwa mwitikio ni mdogo sana kwa wataalamu wa Ugavi na manunuzi katika kuhudhuri mafunzo hayo yanayotolewa na chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam ingali mafunzo hayo ni bure gharama zote zimetolewa na taasisi ya Ugavi na manunuzi ya Kuehne.
"Wataalamu wamesoma lakini teknolojia inakuwa, saivi tunasimu janja ambapo zamani hazikuwepo kwahiyo elimu ni kitu ambacho kinaendelea na kuendelea, hivyo wanataaluma ya ugavi wanatakiwa kujifunza zaidi ili kuwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi kulingana na wakati uliopo." Amesema Dkt. Omary
Dkt. Omary amesema kuwa kwa mwaka huu kutakuwa na Mafunzo mengine ya Ugavi na manunuzi katika sekta ya afya hivyo wataalamu wa kada hiyo wanaaswa kuomba kwani mafunzo yanayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe hapa nchini ni bure yaani gharama zote zimeshagharimiwa na taasisi ya Kuehne.
"Wito kwa wataalamu wa Ugavi na manunuzi ni kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na chuo Kikuu Mzumbe wakishirikiana na taasisi ya Kuehne."
Nae Mshiriki wa Mafunzo hayo, Musa Mrutu amewashukuru Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam pamoja na taasisi ya Kuehne kwa kutoa mafunzo hayo.
Renata Mkinga amesema mafunzo hayo yatasaidi ofisi pamoja na jamii kwa ujumla kwani yanasaidia kutokana na wanavyotoa mifano iliyohai na ambayo imeshawahi kuwepo katika taasisi mbalimbali.. Mshauri na Mkurugenzi wa Medal Investiment, Christopher Msemo na Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu na Mzumbe na Mratibu wa Mradi wa Kuehne Foundation Daktari Omary Swalehe wakiwatunukia vyeti washiriki wa Mafunzo ya Ugavi na Manunuzi katika sekta ya Afya. Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 16, 2021 katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment