Meneja wa Masoko na Uhamaishaji wa Self Microfinance Linda Mshana akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea Banda lao ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha katika maonesho ya Biashara ya 45 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
TAASISI ya kifedha ya Self Microfinance imelenga kuongeza wigo na kuwapa fursa ya kukuza mtaji kwa wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa ili kuongeza ajira kwa watanzania hususani vijana.
Katika maonesho ya biashara ya 45 ya kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam, Taasisi hiyo imelenga zaidi katika kutoa mikopo wananchi,taasisi za kiserikali, asasi za kifedha, Kilimo na biashara.
Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Masoko na Mhamasishaji wa Self Microfinance Linda Mshana amesema taasisi yao wanatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo,wa kati na wakubwa ili waweze kujikuza kiuchumi katika biashara zao.
Mshana amesema, Self Microfinace amesema mikopo hiyo inawawezesha wafanyabishara kukuza mitaji yao sambamba na wakulima.
Amesema, mikopo yao inapatikana kwa masharti nafuu na wanawakaribisha asasi za kifedha kama vikundi vya SACCOS.
Mshana amewataka watanzania kujitokeza katika banda lao lililopo ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha ili kupata maelezo mbalimbali na kufahamu zaidi kuhusu taasisi yao na huduma za kifedh wanazozitoa.
Kwa upande wa Mnufaika, George Buchafwe amesema taasisi ya Self Microfinance imewanufaisha wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia mikopo iliyowawezesha kununua vitendea kazi vitakavyomuwezesha mjasiriamali kujiendeleza kiuchumi.
Buchafwe amesema, kwa kuwawezesha wajasiriamali wameweza kununua mashine mbalimbali kama za kukamulia mafuta ya alizeti.
Amesema, uwezeshaji huo umeongeza soko la ajira, na hata kuongeza pato la Taifa ikwa bidhaa mbalimbali kutengenezwa ndani ya nje na kuacha kuingiza vitu kutoka nje.
Kwa sasa Self Microfinance inapatikana katika ofisi zake zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya na Kahama na pia wanapatakina kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la Self Microfinance.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment