Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa akizungumza .
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo akielezea jambo
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima
NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE
SERIKALI Mkoani Tanga imesema itahakikisha zao la Mkonge linaimarika kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa zitokanazo na zao hilo duniani yanayolenga kuachana na matumizi ya bidhaa za Plastiki ambazo zina athari kwa Jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa miaka mingi nguzo ya uchumi ya Mkoa huo ilikuwa zao la Katani na miaka 50 iliyopita Tanga ilikuwa inazalisha tani 150,000 lakini baada ya marekebisho na nguvu kubwa mkoa wa Tanga inazalisha tani 35000.
Alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu imeweka mkakati wa makusudi wa kuzalisha zao la Mkonge Kitaifa kutoka Tani 35,000 hadi kufikia Tani 120,000.
Aidha alisema mkakati huo unasimamiwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ambao wakuu wa mikoa na wadau wengine wote wamekuwa ni sehemu ya mpango huo mafanikio yake yapo hapa wilayani Korogwe.
Alisema ili kufikia Tani 100,000 za Mkonge wanaweza kufikia huko kwa kushirikiana na wawekezaji wakubwa wakiwemo Mohamed Interprises Limited, Amboni Platation, Kwale, Palet.
Mkuu huyo wa mkoa aliekeza lakini bodi inajua na ina maelekezo ya Waziri Mkuu na Serikali juu ya mkakati huo maana yake wanataka kuwa na uzalishaji wa mkonge mkulima ashiriki kama mmiliki wa uzalishaji huo na sio kama manamba na namna ya kufanya hivyo ni kupitia kwa vyama vya ushirika Amcos kama serikali, Mrajis wa vyama wataanza kuwa na uwezo wa uongozi na rasimali ili iweze kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi.
Alisema vyama vya Ushirika (AMCOS) wana ubia katika uzalishaji na Kampuni ya Sisalana ambayo inamilikiwa na Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) hivyo Sisisala lazima ijengewe uwezo wa kupokea zao linalotoka kwa Mkulima kutokana na kwamba hivi sasa Sisalana wanapokea Tani 6000 kwenye Amcos zote na wana uwezo wa kupokea tani 11000 .
Aliseam hivyo yeye amefika na timu yake kuweza kutengeneza mkakati ili hizo tani 11000 ziwafikie Sisalana na zipate kuchakatwa na mkulima aweze kupata haki yake pamoja licha ya kwamba huko kuna changamoto za pande zote mbili za Amcos na Sisalana na nyengine ambazo lazima utatuzi wake upatikana kwa Serikali ikiwemo suala la miundombinu inayopitisha
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa alisema sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo inawaruhusu kuingia kwenye uwekezaji ndio maana wameshiriki kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa kwenye Corona ambazo zinamilikiwa na Kampuni ya SISALANA ambayo ni kampuni tanzu ya NSSF.
Alisema kampuni hiyo imepewa dhamana ya kuendesha Corona tano kwa madhumuni ya kuweza kurejesha fedha za wanachama ambapo wanaendesha shughuli za biashara hiyo kwa kushirikiana na Amcos kazi yao kubwa ni kuchakata majani ya katani ili Amcos ziweze kuuza brashi ambayo inaitwa Singa na wao wanaweza kupata tozo kwa ajili ya kuchakata.
Alisema hilo limewapelekea kwenye biashara ya mkonge na kwao hiyo haitoshi kuchakata kutokana na kwamba itawachelewesha kurudisha fedha zao wanazotaka kuzipata na pili wanataka biashara hiyo iwe na maana katika kutunishia mfuko wa Pensheni ili waweze kuwa na uwezo mkubwa wa kulipa pensheni kila inapohitajika kwa wanachama wao.
Naye kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo alisema walianza kazi yao kwa kufanya ukarabati katika mitambo katika kiwanda cha Usambara na baada ya hapo watahamia Mwelya ili kuhakikisha mitambo inakuwa katika hali nzuri.
Alisema wakati wanafanya ukarabati na matengenezo kwenye mitambo hivyo wanaomba wakulima wa mkonge wanaosimamiwa na Amcos tano za Mwelya, Magoma, Hale, Ngombezi na Magunga wanaomba wakulima wawape ushirikiano ili waweze kufanya maboresho.
Alisema kwa sababu wanapofanya matengenezo makubwa wanasimamisha uzalishaji kwa muda wa usipoungua wiki mbili mpaka tatau hivyo wanasisitiza kwa wakulima waongeze kasi ya upelekaji wa majani kwa kupeleka awamu mbili ili kuepuka hasara watakazokutana nazo wakati wanaposimamisha uzalishaji kwa siku hizo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment