TAARIFA KUTOKA TUNDURU | Tarimo Blog

 

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, amerejesha jumla ya shilingi 85,463,848 ambazo wananchi mbalimbali waliporwa na watu au taasisi mbalimbali kinyume cha sheria, ofisi ya DC ikafanya oparesheni za kuokoa fedha hizo;

1. Shs 44,272,196 kati ya tzs 55,535,497.69 zimerejeshwa kwa wakulima waliokuwa wameporwa na vyama vya msingi baada ya wakulima kuuza mazao kwa mfumo wa stakabadhi za ghala kisha watumishi wasio waaminifu wa baadhi ya vyama vya msingi kuwadhulumu fedha hizo.

2. Shs 12,000,000 kati ya 96,000,000 alizodhulumiwa Mwalimu Mstaafu Ndg. Yusuph Bakari Yusuph, baada ya kuwa amekopa jumla ya shs 3,300,000 kwa watu wawili binafsi na taasisi moja ya ukopeshaji fedha. Pensheni yake ya Mil 96 ilipoingia kwenye akaunti yake, wafanyabiashara hao wawili na taasisi moja ya ukopeshaji fedha walimteka na kumleta mjini, wakafanya connection benki ya NMB na kumpora tzs 63 Mil na baadaye kwa kutumia kadi yake, kampuni ya ukopeshaji ikachukua tzs 33 Mil kwa nyakati tofauti.

 Haya yalitokia kati ya tarehe 14 - 18 Feb 2019. Mzee aliripoti polisi lakini hakusaidiwa. Miaka miwili baadaye mwezi Julai 2021 amemfikishia suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru na ndipo akachukua hatua na fedha zake zimeanza kurejeshwa baada ya hao waliomuibia kukiri kuwa walimdhulumu.

3. DC Tunduru pia amerejesha Shs 18,381,456 kwa wanachama wa TUNDURU TEACHERS SACCOS baada ya kutapeliwa na viongozi wao, pesa hizi ni 15% tu ya pesa zote wanazopaswa kulipwa. Tunaendelea na kazi ya kusimamia hadi wote walipwe fedha zote.

4. Shs Mil 10,810,186 zimerejeshwa pia kwa wananchi wengine mbalimbali na taasisi za kukopesha pesa na watu binafsi.

Idd Mohammed M,
Tunduru,
19 Julai 2021.




 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2