TOZO ZA MIAMALA KUJENGA MADARASA 10,000 NA KUKARABATI SHULE KONGWE ZA MSINGI 2,100-UMMY I | Tarimo Blog

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

Wizara ya TAMISEMI inakwenda kunufaika na tozo za miamala ,kwa kujenga majengo ya vyumba vya madarasa 10,000 kwa shule za msingi na sekondari nchini ili kupunguza changamoto ya baadhi ya wanafunzi kusoma chini ya mti na mlundikano kwa wanafunzi madarasani.

Pia kufanya ukarabati kwa shule kongwe za msingi 2,100 ,ambazo nyingine zimejengwa kabla ya Uhuru ili kuendeleza mpango wa serikali kuboresha na kuweka mazingira bora kwa wanafunzi.
.
Hayo yalielezwa na Waziri wa TAMISEMI ,Ummy Mwalimu wakati akizungumza katika makabidhiano ya madarasa saba na matundu vya vyoo vya walimu viwili yaliyokarabatiwa na ufadhili kutoka Bilal muslim mission na Lady Fatimah Trust kwenye shule ya msingi Kaole ,Bagamoyo.

Alisema ,zipo shule ambazo wanafunzi hukaa 200-300 katika darasa moja huku akidai kila darasa moja linakaa wanafunzi 45 hivyo wanatarajia kuwexesha wanafunzi 450,000 kuwa darasani.

Pamoja na hayo ,Ummy alieleza kuwa hadi sasa kuna jumla ya uhaba wa madarasa 100,005 kwenye shule za msingi na sekondari hivyo amesema serikali itaanza na madarasa hayo .

Ummy aliwaagiza wakuu wa mkoa kusimamia changamoto za maendeleo na pia amewaelekeza wakurugenzi kutenga asilimia 40 ya makusanyo ya mapato kwaajili ya kutatua masuala ya maendeleo.

" Katika hili tutawapima wakurugenzi wa halmashauri kwa kutenga fedha hizi ,lazima mtenge fedha hizi kwa ajili ya kuondoa kero za maendeleo ,kipaombele ni hicho sio kutenga fedha hizi kwa manufaa yao ama semina "

"Mkeka wa Maded nao unakuja ,tunawapima kwa uwajibikaji " alisisitiza Ummy.

Ummy aliupongeza uongozi wa Bilal Muslim mission

Nae mkurugenzi wa Bilal Muslim mission, Khairumbanu Alibhai alisema ,wameanza shughuli za kuunga mkono juhudi za serikali ikiwa ni miaka 34 sasa .

Alisema ujenzi wa madarasa hayo umekamilika na hadi wanakabidhi umegharimu kiasi cha sh .milioni 70.

Kwa upande wake ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge alieleza mahitaji ya madarasa kimkoa ni 8,900 na yaliyopo ni 4,500 .




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2