WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeanzisha vituo 17 vya atamizi ili kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali zinazowakumba wabunifu wachanga nchini
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Prof. Ndalichako amesema Serikali imedhamiria kuwajengea ujuzi vijana ili bunifu zao wanazozifanya zikawe na manufaa kwa jamii inayowazunguka na hata kutatua changamoto hivyo amewataka kutokata tamaa kwani wanashiriki katika kujenga nchi kwa bunifu zao zenye tija ili waweze kukuza uchumi wa nchi yetu.
“Tuwape fursa, vijana wetu, tuwaamini hasa wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo tusiogope kuwakaribisha tuwape nafasi ili waweze kuonesha ujuzi wao wenye tija." Amesema Prof.Ndalichako.
Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu amesema wamekuwa wakiwafuatili vijana ambao wamepitia mafunzo ya ubunifu kwani lengo lao ni kuwasaidia wabunifu ili waweze kuonyesha mchango wao katika jamii.
“Kupitia ripoti hii aambayo imezinduliwa na kuweza kugaiwa kwa kila mmoja kikubwa kuangalia mchango wa ubunifu hapa nchini upi na kuweza kupata mrejesho kusudi tuweze kuboresha zaidi”. Amesema Dkt.Nungu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment