NBAA, TRA WAKUTANA KUJADILI BAJETI, UCHUMI NA MASUALA YA BAJETI | Tarimo Blog

 


BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA,) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) wameandaa jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu kwa kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) Alphayo Kidata mamlaka hizo mbili zina mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa Taifa na kupitia majukwaa ya namna hiyo wataalamu hao watatoka na mikakati itakayoleta tija katika sekta fedha na uchumi kwa ujumla.

Amesema, kuwa TRA kwa kushirikiana na NBAA wataendelea kukutana na kujadili masuala ya uchumi yatakayoisaidia Serikali katika kujenga uchumi imara na shindani barani Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Taifa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA,) CPA. Pius Maneno amesema, Julai kila mwaka NBAA kwa kushirikiana na TRA huandaa jukwaa maalumu la pamoja na kujadili masuala ya uchumi na kwa mwaka huu jukwaa hilo limelenga kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya kodi kwa kutoa nafasi kwa washiriki kujadili bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 pamoja na kuja na mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/2023.

Amesema kuwa, washiriki pia watapata nafasi ya kujadili sera maendeleo ya Tanzania kwa kulinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na changamoto za kikodi nchini.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na wahasibu na wakaguzi alipokuwa anafungua jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu lenye lengo la kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA na kufanyika katika ukumbi wa APC Bunju leo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza na wahasibu na wakaguzi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua  jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu lenye lengo la kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA na kufanyika katika ukumbi wa APC Bunju leo Dar es Salaam.
Aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya NBAA, CPA Nicholas  Duhia akitoa neno la shukrani mara baada ya Mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata kufungua jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu lenye lengo la kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA na kufanyika katika ukumbi wa APC Bunju leo Dar es Salaam.
Baadhi ya wahasibu na wakaguzi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi alipokuwa anafungua jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu lenye lengo la kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA na kufanyika katika ukumbi wa APC Bunju leo Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata(katikati waliokaa) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno(wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja wahasibu na wakaguzi wa hesabu waliofika kwenye jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu lenye lengo la kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA na kufanyika katika ukumbi wa APC Bunju leo Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata(kulia) akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ufunguzi wa jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu kwa kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi lililoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA) kwa kushirikiana na TRA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza jambo na Mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata(kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa APC  ajili ya kufanya ufunguzi wa jukwaa maalumu la mafunzo  ya siku tatu kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu kwa kujadili masuala ya bajeti, uchumi na masuala ya Kodi.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2