VODACOM YAKAMILISHA KAMPENI YA TWENDE MJINI NA MPESA | Tarimo Blog

Na.Khadija Seif, Michuzi TV


Yakabidhi gari aina ya Toyota cruise kwa Mwanamke

KAMPUNI ya Vodacom imekamilisha Kampeni yake ya 'twende mjini na Mpesa' kwa kuwakabidhi zawadi zao washindi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na pwani wa Kampuni ya Vodacom Brigta stephen amesema tulitoa bajaji moja kila wiki kwa wiki 8 na Leo inatoka gari aina ya Toyota cruise.

"Unapokua na M_pesa inarahisisha Maisha kutokana na kulipia nahitaji mbalimbali luku,umeme kununua bando na vingine vingi hivyo utaona mtandao wetu ilivokua na faida na Leo tumekabidhi pikipiki 5 kwa washindi ,bajaj moja pamoja na gari aina ya Toyota cruise "

Stephen ametoa rai kwa watumiaji ya wa Vodacom kuendelea kutumia mtandao huo vizuri ili waweze kufaidika na zawadi mbalimbali zinazotolewa na Vodacom.

Hata hivyo amewataka waliopokea zawadi hizo kuwa mfano mzuri na kujitangaza vizuri mtandao huo.

Huku Mwakilishi wa Mkuu wa kitengo cha Mkakati kutoka Mpesa Nelusigwe Mwangota ameeleza jinsi gani kampeni hiyo ilikua na lengo la kuwashika mkono wa Tanzania na Kuishi maisha ya kidigitali kutokana na kutumia Mpesa na kuwawezesha kufanya miamala kwa urahisi na kulipia bili mbalimbali.

"Tumeendelea kuwa wabunifu ambapo tumekua tukitatua matatizo mbalimbali tumebuni M_pawa,M_koba,songesha huduma zote hizi ni kwa ajili ya kuwezesha kupata mkopo kwa haraka."

Pia amesema wanawake wamekua wakiachwa nyuma lakini katika kampeni hii haajaachwa mtu tumekuwa pamoja na ndio maana Mshindi wa gari ni Mwanamke.

Promosheni ambayo imechukua jumla ya week 8 katika Mikoa mbalimbali na Leo imefika tamati kwa kuwakabidhi zawadi za washindi wa Mkoa wa Dar es salaam ameongeza Mwangota.

Kwa upande wake aliyeibuka Mshindi wa gari aina ya Toyota cruise mpya 2021 Neema ikolo amewapongeza Kampuni hiyo kwa kuendesha kampeni hiyo ya Twende Mjini na Mpesa ambayo imetimiza ndoto za watu wengi ikiwemo yeye binafsi.

"Mara ya kwanza napigiwa simu sikuamini kabisa nilijua ni matapeli lakini baadae ni kapokea simu nikamsikia salama jabir aliongea ndipo nilipoamini nashukuru Sana Vodacom kwa kampeni hiyo itakayoenda kubadilisha maisha ya wengi Sana hususani watu wenye Hali ya chini."

Hata hivyo Ikolo ameeleza Sababu ambayo anahisi imemfanya kuibuka Mshindi wa gari katika kampeni hiyo.

"Kiukweli Mahitaji yangu yote na manunuzi ya vitu nalipa kwa kutumia Mpesa ndio sababu iliyochangia kushinda kwangu Shindano hili."


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2