Wanafunzi shule ya Joyland watia fora kwa vipaji | Tarimo Blog

Mkurugenzi wa shule ya msingi na sekondari  Joyland zilizoko Toangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, Fredrick Okuku Otieno akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa mbio za marathoni kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika leo Jumamosi na kushirikisha michezo mbalimbali.
Wanafunzi wa shule ya awali Joyland ya Toangoma Kigamboni wa Simba na Yanga wakipambana kwenye soka wakati wa Bonanza la Michezo la shule hiyo leo Ijumaa kwenye viwanja vya shule hiyo.
Wanafunzi wa Green House wa shule ya Joyland wakishuhudia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika Jumamosi kwenye viwanja vya shule hiyo Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Blue House wa shule ya Kimataifa ya Joyland ya Toangoma wakishuhudia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika Jumamosi kwenye viwanja vya shule hiyo Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa shule ya msingi na sekondari  Joyland zilizoko Toangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, Fredrick Okuku akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa mbio za marathoni kwenye Bonanza la shule hiyo.


Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland ya Tuanganoma iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, wametia fora kwenye bonanza kwa kuonyesha vipaji vya aina mbalimbali.

Katika bonanza hilo lililowashirikisha wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Joyland, wanafunzi hao walionyesha umahiri kwenye kuigiza michezo mbalimbali ikiwemo ile kushindana kula haraka.

Miongoni mwa vitu vilivyotia fora kwenye bonanza hilo ni mbio fupi na ndefu, kukimbia na magunia, kuruka viunzi na namna walivyomudu kuwasilisha sanaa hiyo kwa ubunifu mkubwa.

Mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Jonathan Mbogoma, amesema wameandaa bonanza hilo kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya wanafunzi hao kwenye fani mbalimbali na kwamba hufanyika mara tatu kila mwaka.

Amesema mbali na masomo ya darasani shule imeona umuhimu wa kuwakutanisha wanafunzi hao kwenye bonanza ili waonyeshe vipaji walivyonavyo kwenye mitindo ya mavazi, muziki wa bongo fleva na maonyesho ya mitindo ya mavazi.

Ameongeza kuwa watakuwa wakiandaa bonanza kama hilo mara kwa mara kwaajili ya kuvumbua vipaji na kuvilea kwani vinaweza kukua na kuwanufaisha kwenye maisha yao ya baadaye.

“Mbali na masomo ya darasani tumeona kuna umuhimu wa kubaini vipaji vya wanafunzi na kuvikuza mtoto lazima alelewe katika nyanja mbalimbali kwasababu mwisho wa siku anawez kuishi kutegemee kipaji chake.” Amesema.

“Kuna mifano ya wanamuziki wengi ambao wamefanikiwa sana kwenye maisha kutokana na vipaji mbalimbali, mwanafunzi anaweza asifanye vizuri sana darasani lakini akawa na kipaji kitakachompa maisha mazuri sana.” Alisema

Amesema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2015 imekuwa iithamini michezo kwa kufanya mabonanza kama hayo kila mwaka kusaka vipaji.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2