Na PATRICIA KIMELEMETA
WATAALAM wa Manunuzi na Ugavi watakaoshindwa kutoa ushauri mzuri kwenye manunuzi ya vifaa mbalimbali vya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iwe Serikalini au Sekta binafsi watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili au kushushwa madaraja.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB),Shamim Mdee kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere yanayoendelea katika Viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa, kumekua na malalamiko kutoka ofisi mbalimbali ambazo zimewahusisha watalaam wa manunuzi na ugavi kushindwa kutoa ushauri sahihi katika ununuzi wa vifaa vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,hali iliyosababisha miradi hiyo kutekelezwa chini ya kiwango, hivyo basi PSPTB itawachukulia hatua za kinidhamu watalaam wasio waaminifu ili iwe fundisho kwa wengine.
"PSPTB haitawavumilia watalaam wasio waaminifu ambao wanaangalia maslahi yao binafsi na kushindwa kutoa ushauri sahihi kwenye manununuzi na ugavi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iwe Serikalini au Sekta binafsi," amesema Shamim.
Ameongeza kuwa, wataalam hao wwmekuwa wakisababisha hasara kutokana na ushauri mbovu wanaoutoa,jambo ambao Ni kinyume na miiko ya kazi zao.
Amesema hivyo basi PSPTB itaendelea kuwafuatilia watalaam hao popote walipo kwenye ili kujua kama wanasimamia taaluma yao vizuri au la na kuepusha malalamiko yatokanayo na ushauri mbovu.
Amesema kuwa, lakini pia inawakumbusha wataalam hao kulipa ada zao za uanachama kwa kutumia mfumo wa mtandao ili waweze kuendelea na usajili wao.
"Hakuna haja ya kuja ofisini, kila kitu kipo kwenye mtandao wanaweza kuingia na kujisajili ili walipe ada zao za uanachama kwa sababu mwaka mpya wa serikali umeanza," amesema.
Shamim amesema kuwa, lakini pia katika kipindi hiki ambacho wanashiriki maonyesho ya sabasaba, watalaam hao wanaweza kujitojeza kwenye banda lao kwa ajili ya kupata maelekezo mbalimbali ikiwamo ushauri na usajili.
Watumishi wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi(PSPTB) wakitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho ya sabasaba
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment