Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dr Faustine Ndungulile akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo (kulia) alipotembelea baada la Shirika la Posta Tanzania (TPC) baada ya kuzindua huduma mtandao leo katika Maonesho ya Biashara ya 45 ha Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dr Faustine Ndungulile akizungumza na watendaji wa Posta na TANTRADE wakati wa kuzindua huduma mtandao itakayokuwa inapatikana kupitia Shirika la Posta Nchini (TPC) Leo katika Maonesho ya Biashara ya 45 ha Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa TANTRADE
Edwin Rutageruka baada ya kuingia makubaliano ya pamoja ya kushirikiana katika mfumo wa kidigitali wa Duka Mtandao uliozinduliwa leo na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr Faustine Ndungulile.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr Faustine Ndungulile ametoa rai kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kufanya biashara zao kidigitali kwa kutumia Shirika la Posta Nchini (TPC)
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa duka la mtandao chini ya TPC katika Maonesho ya Biashara ya 45 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Ndungulile amesema kwa kutumia Shirika la Posta, wafanyabashara wanaweza kujitangaza kitaifa na kimataifa kwa sababu Shirika la Posta limejisajili kimataifa zaidi.
Amesema, huduma hii itamsaidia mwananchi yoyote kuagizia kitu mtandaoni na kukipata kwa kwa wakati kwa sababu Shirika la Posta watachukua jukumu la kusafirisha mzigo huo hadi kwa mteja.
"Tumeingia makubaliano na TANTRADE kuwaomba wafanyabiashara, wajasiriamali na wenye viwanda kujiunga na Huduma hii ya duka mtandaoni ambapo wataweza kujitangaza kitaifa na kimataifa kupitia Shirika la Posta."Amesema Ndungulile.
Amesema, Shirika la Posta limejizatiti kuboresha huduma zake na kuwa kidigitali zaidi na sio kuuza stempu za barua na kusafirisha vifurushi pekee na wanataka Posta iwe kitovu cha biashara mtandao ndani ya nchi.
Aidha, Ndungulile amesema Shirika la Posta limeanzisha huduma mpya ambayo inaitwa huduma Pamoja Centre ambayo inatarajia kuwa na taasisi 13 za kiserikali zitakazokuwa zinatoa huduma ndani ya ofisi za Posta.
"Huduma Pamoja Centre itawasogeza watanzania karibu sababu taasisi 13 zitakuwa ndani ya ofisi moja na hili limeanza mwezi huu Julai na tumeanzia Dodoma na Dar es Salaam na tutaenda nchi nzima" Amesema.
Ndungulile amewapongeza Posta kwa mabadiliko makubwa wanayoyafanya na kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa kidigitali na kusogeza huduma karibu na wananchi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment