Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
BENKI ya Akiba (Akiba Commercial Bank) imezindua huduma mpya ya Akiba Wakala ambayo itamuwezesha mteja wa Benki hiyo kupata huduma kwa kufanya miamala mbalimbali bila kufika kwenye tawi lolote la Benki hiyo kote nchini.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Mkuu, Kitengo cha Biashara katika Benki hiyo, Wenster Kaunga amesema huduma hiyo itawasaidia wateja hao kote nchini kuondoa changamoto ya kufika kwenye matawi mbalimbali ya Benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za Kibenki.
“Huduma hii imezinduliwa leo, tunaamini wateja wetu watapata fursa kuwatembelea Mawakala walio karibu na wao ili kupata huduma hizi”, amesema Kaunga
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Benki ya Akiba, Dora Saria amesema kwa sasa wameanza na Mawakala 200 nchini kote, amesema huduma hiyo itawasaidia Watanzania kupata huduma hizo za Kibenki kwa hara na urahisi.
Dora amesema Benki hiyo imeingia ubia na Benki ya Taifa ya Malawi (National Bank of Malawi) katika kupanua ukubwa wa kibiashara katika ukanda wa Afrika. Pia Benki hiyo imeanza mkakati wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma zake kupitia Akiba Mobile.
Meneja Mkuu, Kitengo cha Biashara katika Benki ya Akiba, Wenster Kaunga (wa pili kutoka kulia) akizindua huduma hiyo ya Akiba Wakala ambayo itapatikana nchini kupitia kwa Mawakala wake.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment