Na Pamela Mollel, Arusha
Chuo cha uhasibu Arusha IAA kimeanza ujenzi wa miradi ya zaidi ya bilioni 15 kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji elimu chuoni hapo.
Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua miradi hiyo naibu waziri wa fedha na mipango Hamad Yussuf Masauni, alisema ameona majengo kadhaa yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa yanaendelea kujengwa yakiwemo ya maktaba, mabweni, sehemu ya chakula na sehemu ya kujisomea (Vimbweta).
kwa upande wa jengo la chakula litagharimu zaidi ya Sh.bilioni 1.3 na linatarajia kukamilika Oktoba mwaka huu.
Alisema katika majengo mengine kutakuwa na kituo cha ukuzaji na uendelezaji wa biashara na kitengo cha TAHAMA ambayo yapo katika hatua nzuri ya ujenzi.
"Miradi hii muhimu kwa wanafunzi wetu kama ujenzi wa mabweni, utakapokamilika utasaidia wanafunzi hususani watoto wa kike, kuendelea na masomo, lakini pia kwa chuo watapata kipato cha pango watakazolipa na kujiletea maendeleo ya chuo"alisema.
Aidha alisema serikali iko tayari kuongeza nguvu kwa yale maeneo ambayo watahitaji msaada ili kuongeza kasi ya kuwaandaa wanafunzi kuwa tayari kwaajili ya maisha yao na wahitimu wanaomaliza fani mbalimbali chuoni waweze kujiajiri na kujiendeleza wenyewe, badala ya kusubiri kuajiriwa.
"Tuna waunganisha wanafunzi wetu na makampuni ya umma pamoja na Taasisi binafsi za masuala ya kodi, masuala ya benki kwa sababu soko lake ni zuri nchini, kwani maeneo haya mazuri yanatengeneza fursa kwa vijana wetu wa kitanzania za kujiajiri,"alisema.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka alisema kwasasa chuo kinatekeleza miradi itakayowezesha wanafunzi kupata elimu kwa ufanisi zaidi, mbali na madarasa, maktaba, sehemu za kulia chakula na mabweni lakini pia utengenezaji wa vimbweta vyenye mfumo wa umeme lakini pia uwepo wa mtandao(Internet) vita waweze kusoma kwa urahisi.
"Tunatarajia Oktoba mwaka huu wanafunzi wataongezeka kutokana na chuo kuongeza baadhi ya fani lakini pia uboreshaji huu tunaoufanya,"alisema.
Prof.Sedoyeka alisema ujenzi wa bweni unoendelea chuoni hapo, kwa awamu ya kwanza ambao utakamilika mwezi oktoba mwaka huu unakadiriwa kubeba wanafunzi 2000 huku matarajio ni kufikisha wanafunzi 5000 ifikapo mwakani.
"Tunaalika wenye nyumba karibu na chuo chetu ambao wanania ya kugeuza majengo yao kuwa mabweni, kwani tutayakagua na tukijiridhisha tutawaweka wanafunzi wetu huko" aliongeza.
Sambamba na hilo alisema kitengo Cha ubunifu kwa wanafunzi, ni mpango endelevu na wanafunzi wote watalazimika kuja na wazo la kibiashara Ili kuwaandaa wataalamu wabobezi watakaoendana na soko la ajira.
Picha ya pamoja ya watendaji wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Mhandisi Hamad Yussuf Masauni mara baada ya kutembelea ujenzi wa miradi mbalimbali chuoni hapo.
Naibu waziri wa fedha na mipango Hamad Yussuf Masauni akimwagilia maji mti Mara baadaye ya kuupanda ikiwa ni sehemu ya ishara ya kumbukumbu alipotembelea ujenzi wa miradi chuo cha uhasibu Arusha (IAA).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment