Benki ya NBC imeendelea kuongeza juhudi za kuwafikia Watanzania katika kila kona ya nchi kwa dhumuni la kujenga jamii yenye uchumi shirikishi, juhudi zinazoenda sambamba na malengo Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za kibenki.
Benki hiyo imefanya hivyo kupitia huduma yake ya NBC Wakala Plus kwa kufungua tawi ya wakala mkuu katika Mtaa wa Mama Madaba, Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali.
Hatua hii imefanyika miezi kadhaa baada Benki ya NBC kuzindua tawi kama hilo la NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi na kuleta manufaa kwa wajasiriamali na wananchi wa mkoa huo.
Pamoja na kusogeza huduma za kibenki kwa wananchi, NBC Wakala Plus pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbali mbali za kibiashara pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara, waajiriwa na wakulima wa mkoa huo.
Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudh weee uria hafla ya uzinduzi wa NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace Quintine ameipongeza Benki ya NBC kwa kuona fursa kubwa wilayani humo zinazotokana na shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazofanywa na wananchi.
Grace amesema benki hiyo imefanya uwekezaji wake na kutoa elimu kwa wakulima na wajasiriamali wa wilaya ya Mbinga na kwamba Benki ya NBC imeonyesha mfano wa kuigwa wa kutoa elimu kwanza kabla ya kuleta huduma hali inayopelekea wakazi wa Mbinga kutumia huduma za kibenki kikamilifu ili kuwaletea maendeleo.
Aidha, Grace pia ameishukuru benki hiyo kwa msaada wa mabati 240, mifuko 120 ya saruji na kilo 30 za misumari ya bati katika kuchangia juhudi za kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Nazareth iliyopo Wilaya ya Mbinga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Elibariki Masuke amesema kuwa uzinduzi wa Wakala Mkuu wa NBC Mbinga ni moja ya mikakati ya benki hiyo ya kupanua na kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi kwa wananchi hasa katika maeneo yanayokua kiuchumi.
“NBC inaamini kwamba mpango wa upandaji wa mawakala wakuu katika maeneo yenye uchangamfu wa kiuchumi utaongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wananchi na kuinua kipato cha wajasiriamali. Mchakato wa NBC Wakala Plus unaenda sambamba na malengo ya serikali yetu ya kusogeza huduma bora kwa wananchi kwani mawakala wetu wakuu watatoa huduma kama zile zinazotolewa katika matawi yetu yalioenea nchi nzima.” amesema Masuke.
Aidha kwa upande wake, mmiliki wa ofisi hiyo ya NBC Wakala Plus, Agasto James ameishukuru Benki ya NBC kwa kumpa fursa hiyo ya kipekee itakayomuongezea kipato pia kuwa wakala mkuu inampa fursa mbali mbali kwa wakazi wa Mbinga hasa wale watakaotumia ofisi yake kupata huduma mbali mbali zikiwemo kuweka, kutoa, kupokea na kuhamisha fedha, kufungua akaunti mbali mbali na kupata kazi mbali mbali za kibenki pamoja na kufanya malipo na kodi za serikali kupitia mfumo wa GePG.
Kabla ya uzinduzi wa NBC Wakala Plus Wilayani humo, Benki ya NBC iliendesha semina kwa makundi mbali mbali ya wajasiriamali kwa dhumuni la kutoa mafunzo ili kuwasadia wajasiriamali hao kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi. Kupitia semina hizo, Benki ya NBC pia ilipata fursa ya kutambulisha bidhaa zake na kuwaelimisha wajasirimali hao juu ya faida na manufaa ya bidhaa hizo.
Pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa semina hizo pia zililenga viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) Wilaya na Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Mafunzo kwa wakulima yalilenga kufafanua zaidi huduma ya #NBCShambani inayowalenga wateja wanaoshughulika katika sekta ya kilimo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace Quintine (wanne kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa o fisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya Benki ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma yenye lengo yakuwafiki a na ku wa sogeza huduma za kibenki kwa wananchi na wateja wake . Wengine kwenye picha ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke (w anne kulia ) na Wakala wa Ofisi hiyo , Nd. Agasto James (watatu kulia ) na wengine ni maofisa kutoka Benki hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment