Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere (kushoto) akifuatiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa Wise Mgina pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sunday Deogratias (aliyevaa koti na barakoa) sambamba na kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe na wilaya hiyo wakiwa nje ya jengo la maabara katika shule ya sekondari Ikovo iliyopo katika kata ya Ludende wilayani humo.
Kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa ikipatiwa maelekezo juu ya jengo jipya la maabara katika shule ya sekondari Ikovo iliyopo katika kata ya Ludende
Moja ya darasa ambalo kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa imepita kukaguwa katika shule ya msingi Figanga ambapo kuna ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ambapo kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi huo na kushauri kufanya marekebisho madogo madogo.
Jengo la maabara ya shule ya sekondari Mavala iliyopo katika kata ya Milo ambapo kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa ilifika katika maabara hiyo ikiwa imeongozana na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ukaguzi wa miradi mbalimbali.
Kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe ikiwa sambamba na kamati ya siasa ya wilaya ya Ludewa pamoja na viongo wa serikali wakiwa katika harakati za ukaguzi wa miradi mbali ya maendeleo wilayani humo.
Kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe ikiwa sambamba na viongo wa serikali ya wilaya ya Ludewa wakiwa katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala (mwenye nguo za kijani) akizungumza na viongozi wa serikali pamoja na kamati ya siasa ya wilaya ya Ludewa walipotembelea maabara ya shule ya sekondari Ikovo iliyopo katika kata ya Ludende wilayani humo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe akiwa sambamba na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa na wilaya akizungumza baada ya kufanyika ukaguzi wa miradi mbalimbali na kujiridhisha nayo. Kulia ni katibu wa ccm mkoa huo Amina Imbo na kushoto ni mwenyekiti wa ccm wilayani humo Stanley Kolimba.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment