Mwandishi Wetu
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemaliza mgogoro wa muda mrefu wa Kanisa la Sloam, linalojulikana kama Huduma ya Kimataifa ya Siloam (Siloam Ministry International) dhidi ya aliyekuwa mmoja wa makuhani wa kanisa hilo, Elisha Eliya aliyekuwa amepora mamlaka ya kanisa hilo kunyume cha taratibu.
Mgogoro huo ulianza baada ya kifo cha mwanzilishi wa kiongozi mkuu wa huduma hiyo, Mtume na Nabii Nduminfoo Zebedayo Munuo, kwa jina maarufu Eliya na Adam wa Pili au Munguwa Majeshi aliyetwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, ambapo Elisha Eliya ambaye alijipa madaraka ya kumrithi kiongozi huyo bila kufuata utaratibu wa Katiba yake.
Kutokana na hatua hiyo ya kujipa madaraka, Elisha Eliya maarufu kama Miaka 1000, kulisababisha mgawanyiko wa waumini ambapo aliwashawishi baadhi waliomuunga mkono na wakapora mali mbalimbali za huduma yakiwemo majengo ya ibada na kuondoka na ibada.
Pia Miaka 1000 alijaribu kutaka kubadili usajili wa huduma hiyo kwa jina la The Pool of Sloam Church Kanisa la Siloam lakini akakwama.
Kutokana na matukio hayo Bodi ya Wadhamini ililazimika kumshtaki Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya madai namba 24 ya mwaka 2007.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyosomwa na Jaji Leila Mgonya Julai 23,2021, baada ya kusikiliza kesi hiyo upande mmoja kwani mdaiwa hakufika mahakamani, ilikubaliana na maelezo ya wadai na ikatoa amri walizokuwa wakiziomba.
Katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu ilitoa amri za zuio la kudumu dhidi Elisha Eliya, mawakala wake, watumishi wake na mtu yeyote atumikae kwa niaba yake kutokutumia na kutokusajili jina la The Pool of Siloam Church au Kanisa la Siloam mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia mahakama imeamuru kuwa Elisha Eliya, Miaka 1000 kwa kuwa hakuwa kiongozi wa Kikatiba SMI na haruhusiwi kufanya shughuli za kiutawala zikiwemo kuwateua au kuaji ri makuhani au waumini na kuwahamisha kwa jina la The Pool of Soam Churchht.
Vilevile mahakama imemuamuru Elisha Eliya Miaka 1000 au yeyote anayetumika kwa niaba yake kukabidhi mara moja, maeneo, viwanja, majengo na mali zote za SMI walizokuwa wanazitumia kwa jina la SMI au The Pool of Siloam Charch na kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Kaika kesi hiyo Bodi ya Siloam iliwakilishwa na mawakili tofautitotofati katika hatua mbalimbali akiwemo Jerome Msemwa, mon Ndunguru na Salha Mlilima aliyehusika katika hatua ya mwisho ya usikilizwaji wa ushahidi.
Mdaiwa, Miaka 1000 aliwakilishwa na ambaye alijitoa mwaka 2019 wakati kesi ikiwa katika hatua ya usuluhishi ambao ulikwama mbele ya Jaji John Mgetta, baada ya Miaka 1000 kukataa kwenda mahakamani kwa ajli ya usuluhishi.
Awali Miaka 1000 kupitia kwa wakili wake Sweetber Nkuba aliwasilisha maelezo yake ya utetezi wa maandishi,
Katika maelezo hayo alikana madai yote ya mdaia, akidai kuwa hakukaa kutii maelekezo ya Serikali na kwamba wala hapakuwepo na ukiukwaji wa Katiba ya Siloam kama ilivyoelezwa na mdai.
Zaidi alidai kuwa hapakuwepo na aina ypouote udhalilishaji kutokuwa na immani wala dhidi ya mdaiwa na kwamba mdai anapaswa kuthibitisha madai yake hayo.
Hata hivyo mamelezo hayo ya maandishi ya mdaiwa yalitupiliwa mbali na Mahakama Machi 27, 2020 baada ya mdaiwa kutokufika mahakamani wakati wa usuluhishi, hivyo mahakama ikaamuru kesi kuendelea na usikilizwaji wa upande mmoja.
Katika usikilizwaji huo mdaiwa alithibitisha kesi yake kupitia kwa wakili mmoja tu Thebeti Eliya, Kuhani wa Siloam, ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa SMI.
Kwa mujibu wa maelezo ya wadaiwa, Huduma ya Siloam Ministry International (SMI) ilianzishwa na kuongozwa na Mtume na Nabii N.Z Munuo, maarufu kama Eliya, Mungu wa Majeshi, mwaka 2003.
Huduma hiyo ilisajiliwa na Serikali ya Tanzania, Wizara ya Mambo ya Ndani kwa hati namba SO.12880 iliyotolewa Agosti 9, 2005, ambapo ilieneza Injili ya Yesu Kristo na kujenga makanisa maeneo mbalimbali nchini.
Tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2003 hadi mwanzilishi huyo alipotwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, huduma hiyo ilikuwa imeshakubalika ndani na nje ya nchi, ambapo kazi ilipanua na kujenga vituo vya huduma katika mikoa mbalimbali nchini na habari zake zilienea mpaka nje ya nchi.
Kwa muda wote huo kabla ya kutwaliwa kwa mwanzilishi wake, kulikuwa na mshikamani amani na heshima miongoni mwa waumini na viongozi na hapakuwepo na dalili zozote za uvunjifu amani katika kanda zote Saba za huduma hiyo zilizokuwa zimeanzishwa.
Mwaka 2007 aliingia katika huduma hiyo muumini aitwaye Elisha Eliya Miaka 1000, au Nathanile Zabuloni Rusomo akiwa na matatizo mbalimbali ambapo alifunguliwa aliombewa na kufunguliwa kisha akajiunga na huduma ya Siloam Bible School ambapo alifundishwa utumishi.
Wakati tayari akiwa kuhani wa kanda ya Dar es Salaam Miaka 100o alisaliti kiapo cha utumishi, kwani baada ya kiongozi mkuu wa huduma hiyo kutwaliwa na kabla ya mchakato wa kumpata kiongozi mwingijne, yeye alijivua safu ya ukuhani na akajipa cha Mzeituni, Mpaka Mafuta, Mzee wa Siku, Wakili wa Mungu, mungu aliyetuma wote, baba wa uzao, baba halisi nk.
Mpaka aliacha kabisa imani aliyoikuta Siloam na aliazimia kupora thamani, uzuri na kibali cha kusanyiko la Sloam akiwa kwenye majengo ya Sloam.
Aliwapindua waumini kwa kuingiza mafundisho yaliyoacha maswali na hadithi za Kanisa Halisi la Mungu baba. Miaka 1000 alitumia mbinu mbalimbali za kuvuruga kwa kutumia kanuni ya (kugawanya kisha kutawala) safu za makuhani mikoani ambapo aliwashawishi waungane naye kusaliti maono ya mwanzilishi wa SMI.
Ili kuhalalisha mapinduzi hayo alitunga Katiba yake akitaka kusajili The Pool of Siloam Church lakini hakuweza kupitishwa na Serikali kwa kuwa hakuwa mmoja wa viongozi wa Kikatina. Hivyo alizalisha mzozo ili Serikali ifute usajili halali.
Hata hivyo hilo nalo halikufanikiwa japo alitumia njama za kiharamia kama zilizosababisha viongozi wa SMI kuwekwa rumande, kuwatishia maisha yao pamoja na makuhani waaminifu katika huduma ya SMI.
Hivyo yeye na kundi lake la waumini aliofanikiwa kuwashaiwishi katika vituo mbalimbali waliendelea kutumia mali na majengo ya SMI kufanya ibada na kuondoka na sadaka.
Serikali, viongozi na makuhani waaminifu walijitahidi kunusuru mgogoro huo lakini Miaka 1000 alikataa utengamano kwa madai kuwa yeye ni Mungu baba na hawezi kujadiliwa, kuhojiwa wala kushauriwa.
Mahakama katika uamuzi wake ilisema kwa kulingana na ushahidi ni jambo la ajabu ni kwa namna gani mdaiwa aliweza kujichukulia madaraka bila kufuata mchakato wa Kikatiba kama inavyotakiwa.
Mahakama hiyo ilisema kuwa kitendo cha mdaiwa kupora madaraka ya uongozo katika jamii iliyostaarabika ya kidini kama hiyo hakikubaliki na kwamba kwa kitendo hicho alisababisha mkakanyio na hali ya kutokuelewana na mgawanyiko miongoni mwa waumini na na viongozi kwa kuwaondoa katika kusudi la msingi la kuhubiri, kufundisha maelekezo ya Mungu na huduma kwa waumini.
Mahakama hiyo imeonya kwamba viongozi wa kidini hawapaswi kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani badala yake wahimize amani na umoja.
Mahakama hiyo imetoa wito kwa wana Siloam kurejea na kufanya kazi pamoja kama timu bila kujali tofauti zao zilizopita bali wajielekeze kwenye agenda yao kuu ya kuhubiri injili na kuwafundisha waumini matendo mema ambayo yanamvutia Mwenyezi Mungu.
Hivyo ilisema kuwa kutokana na maelezo hayo mahakama inaamua kuwa mdai anastahili amri alizoziomba na kwamba mdaiwa alivamia majengo ya Mdai na kuweka mabango katika makanisa ya mdai Dar es Salaam, Dodoma, Njombe, Arusha Manyara na mahali kwingineko nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment