MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA WILAYANI TANGANYIKA | Tarimo Blog
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua kiwanda cha kuchambua pamba cha NGSInvestment Company Limited kilichopo Kifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, Agosti 26, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Emmanuel Njalu, wa tatu kulia ni Mbunge wa Mpanda V ijijini, Suleiman Kakoso na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavu, Beda Katani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uchambuaji wa pamba kutoka kwa Emmanuel Njalu (wa pili kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo Ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi baada ya kuzindua kiwanda hicho, Agosti 26, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uchambuaji wa pamba kutoka kwa Emmanuel Njalu (wa pili kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo Ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi baada ya kuzindua kiwanda hicho, Agosti 26, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo Kifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi wakati alipowasili kiwandani hapo kuzindua hiwanda hicho, Agosti 26, 2021. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Emmanuel Njalu na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua, Mrindoko. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, Emmanuel Njalu (kulia) wakati alipozindua kiwanda hicho, Agosti 26, 2021. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwananvua Mrindoko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba ambayo imechambuliwa na kufungwa tayari kwa kuuzwa wakati alipozindua kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS Investment Company Limited kilichopo ifukutwa wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi Agosti 26, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Emmanuel Njalu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment