Na Farida Saidy Morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale anashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,100 mali ya halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Muslimu amesema hayo leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake.
Muslimu amesema kutokana na wizi huo watu wengine saba wanashikiliwa na wanadaiwa kushirikiana na Mkurugenzi huyo na wanaendelea kuhojiwa.
Aidha Kamanda Muslim amesema wizi wa mabati hayo ulifanyika Juni 17, 2021 eneo ya ujenzi kitongoji cha Mvumi B wilayani Kilosa katika stoo ya halmashauri hiyo ambayo haikuvinjwa ambapo stoo hiyo haikuvunjwa.
Awali Mwambambale alikuwa mkurugenzi wa halmamshari ya Kilosa kabla ya kuhamishwa halmashauri ya Gairo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment