ASSEMBLE, DAMU SALAMA WACHANGIA DAMU NA KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE | Tarimo Blog

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
Kampuni ya Bima ya AAR na Taasisi ya Damu Salama zimeshirikiana kuchangia damu katika eneo la Bugurini-Chama jijini Dar es Salaam, ikiwa kama sehemu ya kujitolea kwa jamii katika kusaidia wahitaji wa damu salama nchini.

Taasisi hizo ambazo ni wadau muhimu wa sekta ya afya nchini pia zilitoa huduma ya kupima afya za wakaazi wa eneo hilo bure na kutoa huduma nyingine za kitibabu ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitaalam kuhusu afya.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Mkuu wa kitengo cha mauzo na biashara wa Kampuni ya Bima ya Assemble, Bi. Hamida Rashid alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utamaduni wa taasisi hizo wa kujali afya ya jamii na kushiriki kwa vitendo kuboresha na kulinda maisha ya jamii.
"Tukiwa kama wadau muhimu katika sekta ya afya, tumeonelea ni vyema kushiriki katika utoaji wa damu kwa kushirikiana na Damu Salama katika kuokoa maisha ya wanajamii wenye uhitaji sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi wetu, Mh. Samia Suluhu Hassan, za kupunguza vifo vitokanavyo na upungufu wa damu” Alisema Bi Rashidi

"Tunafahamu mahitaji makubwa ya damu salama na ni jukumu letu , ndo sababu kampuni yetu ya Bima ya Assemble kwa kushirikiana na wadau wenzetu (NBTS) tumeonelea tushiriki kikamilifu katika utoaji wa damu" Aliongeza Bi Rashidi

Aidha, Bi. Hamida alisema kuwa taasisi hizo zimetoa huduma nyingine za afya ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitabibu kwa wakaazi wa Mombasa-Ukonga kwani wanaamini kuwa jamii inapaswa kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya kujikinga na magonjwa na kuimarisha afya zao ili kupunguza idadi ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa yatokanayo na kutozingatia au kutofahamu masuala ya msingi ya kuimarisha afya zao.
 
Kwa upande wake mtaalam mwelekezi wa uchangiaji damu kutoka Damu Salama, Bi. Mariam Juma alisema kuwa pamoja na kuchangia damu, taasisi hizo zimetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu namna bora ya kuimarisha afya zao, faida ya kuchangia damu na kuhuisha usalama wa damu ili kuongeza upatikanaji wa damu salama.

Pia alitoa wito kwa makampuni ya ndani na ya umma Ikiwa ni pamoja na watu binafsi kuchangia damu kwa wahitaji ili kuokoa maisha na Kuboresha uchumi wa nchi.
"Pia naomba kutoa wito kwa kampuni za umma na za binafsi na hata watu binafsi kujiunga katika kampeni ya kuchangia damu ambayo itaokoa maisha ya Watanzania wengi wenye uhitaji hivyo kuboresha maendeleo ya nchi" Alihitimisha Bi. Juma

Bwana Abdallah Goboka, mmoja wa wakazi wa Chama- Buguruni ambaye ni mmoja ya washiriki katika uchangiaji damu alizipongeza taasisi hizo kwa jinsi zilivyoendesha zoezi hilo kwa kutoa elimu iliyomuongezea sababu zaidi za kuchangia damu.
 
Assemble Insurance awali ilijulikana kama AAR Insurance ni miongoni mwa Kampuni kubwa na zenye mafanikio zaidi ya Bima Afrika Mashariki na zinazofanya Shughuli zake nchini Tanzania, Kenya, na Uganda. Huduma zetu pia zinafika Rwanda, Burundi, na Sudani Kusini kupitia washirika wetu.

Tumekuwepo kwa zaidi ya miaka 35 huku tukiwa na uzoefu katika bima ya matibabu na jumla, Programu ya Ustawi wa Wafanyikazi na Uokoaji kwa wateja kuanzia mashirika makubwa hadi watu binasi na familia.
Assemble Tanzania ina ofisi zake, Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Zanzibar, na Dodoma. Ikiwa na zaidi ya wanachama 300,000 huku zaidi ya wanachama 40,000 wakiwa nchini Tanzania.






Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2