Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Njombe (NJOREFA) Daktari Thobias Lingangala,ameichangia timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe inayoshiriki ligi daraja la pili kiasi cha milioni 10 ili kusaidia mchakato wa usajili wa wachezaji wa club hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hicho kwa mkuu wa mkoa wa Njombe,amesema lengo la kutoa mchngo huo ni kuendelea kuona timu hiyo inafanya vizuri katika michezo huku akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitoa kwa ajili ya hiyo.
“Timu yetu ya Njombe mji ipo kwenye usajili,na usajili hata kama unataka wachezaji wa ndani huwa inahitajika ghalama kidogo na mimi siku zote nimekuwa nikiwasaidia kuchangia kwenye usajili wao,niwaombe na wadau wengine wachangie kwasababu ni timu yetu”alisema Lingangala
Aidha amesema kutokana na matatizo ya kiuchumi pamoja na kuwahudumia wachezaji kwa ukaribu huku mkoa huo ukiwa na vipaji vingi wameupokea ushauri wa mkuu wa mkoa wa Njombe wa kuweza kujikita zaidi kwenye usajili wa wachezaji wa ndani ya mkoa.
“Mkuu wetu wa mkoa amesema mkoa wake una vipaji vingi kwa hiyo ametushauri kusajili wachezji kutoka kwenye mkoa wetu kwa kuwa vipaji vipo na inakuwa ni rahisi sana kuwahudumia”aliongeza Lingangala
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amemshukuru Dkt,Lingalangala kwa msaada huo kwakuwa muda mfupi ujao timu mbali mbali zinaingia kwenye mashindano.
“Muda mfupi unaokuja tutakuwa na mashindano ya ligi mbali mbali na timu yetu ya Njombe mji itakuwa inashiriki mashindano ya ligi daraja la pili na Dkt,Lingala ngala amekuwa ni msaada mkubwa nichukue nafasi hii kumshukuru kwa kazi mbali mbali anazofanya na niwahamasishe wananjombe tuione njombe mji ni timu yetu na tuone wajabu wa kuisadia kupata wachezaji wazuri na wenye vipaji”alisema Rubirya
Aidha amesema matarajio yake ni kuona mkoa wa Njombe unakuwa na timu nyingi zenye ubora zitakazowakirisha mkoa wa Njombe katika mashindano mbali mbali.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya akipokea fedha kiasi cha milioni 10 kwa ajili ya kusaidia zoezi la usaji wa wachezaji kutoka kwa mwenyekiti wa NJOREFA Dkt,Thobias Lingalangala.Mkuu wa mkoa wa Njombe akizungumza na viongozi wa michezo mara baada ya kupokea fedha kwaajili ya usaji wa timu ya Njombe mji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment