MUUNGANO WA AZAKI ZA UCHECHEMUZI HUDUMA ZA HALI YA HEWA, NISHATI JADIDIFU WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI | Tarimo Blog


Ofisa Mwandamizi wa Ufuatiliaji na Utathimini wa Taasisi ya Can-Tanzania Jackline Massao akifafanua jambo leo Agosti 13,2021 kwa wadau wa warsha ya kuweka mikakati ya uchechemuzi na utekelezaji wa masuala yanayohusu huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu.Warsha imratibiwa na Muungano wa AZAKI za uchechemuzi wa Huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu unaoratibiwa na AZAKI ya CAN Tanzania
Mtalaam wa masuala ya Rasilimali za Nchi na Mabadiliko ya Tabianchi Abdallah Henku( aliyesimama) akitoa maelekezo wakati wa warsha ya wadau kuhusu mikakati ya uchechemuzi na utekelezaji wa masuala yanayohusu huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu.Warsha hiyo ambayo imeandaliwa na taasisi ya Climate Action Network -Tanzania(CAN-TANZANIA) imefanyika leo mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau walioshiriki warsha iliyohusu mikakati ya uchechemuzi na utekelezaji wa masuala yanayohusu huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu wakwa wamenyoosha mikono wakati warsha hiyo ikiendelea.
Tatu Kayumbu(kushoto) kutoka Taasisi ya Wanawake Viongozi katika Kilimo na Mazingira Tanzania(TAWLAE) akiwa makini kufuatilia majadiliano wakati wa warsha hiyo.
Jamali Sagala wa Shirika la Pakaya Culture and Enviromental Group(wa kwanza) akiwa amenyoosha mkono wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Climate Action Network -Tanzania(CAN-TANZANIA) imefanyika leo mkoani Dar es Salaam.
Sivanus Kessy kutoka Shirika la Kuhifadhi Mazingira Duniani(WWF) akitoa mchango wake wakati wa warsha ya wadau wa mazingira walipokutana kufanya uchechemuzi na utekelezaji wa masuala yanayohusu huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu wakwa wamenyoosha mikono wakati warsha hiyo ikiendelea.
Ofisa Sera, Utafiti na Ubunifu Mkombozi Joannes(katikati) kutoka  na Climate Action Network -Tanzania(CAN-TANZANIA) akitoa maoni yake wakati wa warsha hiyo iliyofanyka leo mkoani Dar es Salaam.
Mshiriki wa warsha hiyo Tulinagwe Malopa ambaye ni Ofisa Mawasiliano na Matukio kutoka Nukta Africa akiwa makini kufuata majadiliano wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Climate Action Network -Tanzania(CAN-TANZANIA) imefanyika leo mkoani Dar es Salaam.
Mtalaam wa masuala ya Rasilimali za Nchi na Mabadiliko ya Tabianchi Abdallah Henku akifafanua jambo wakati wa warsha ya wadau kuhusu mikakati ya uchechemuzi na utekelezaji wa masuala yanayohusu huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu.
Msaidizi wa Sera na Utafiti kutoka Climate Action Network -Tanzania(CAN-TANZANIA) Miriamlisa Kasanga akifutiliana majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye warsha hiyo.
Benard Mkwizu kutoka Taasisi ya SMECAO Fund(katikati) akionesha jambo kwenye Laptop wakati majadiliano hayo yaliyowakutanisha wadau kutoka taasisi mbalimbali zilizojikita kwenye mazingira na mabadiliko ya tabianchi.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV  

MUUNGANO wa AZAKI za uchechemuzi wa Huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu unaoratibiwa na AZAKI ya CAN Tanzania chini ya mradi wa "Maendeleo endelevu yanayo zingatia makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na matumizi ya nishati jadidifu" unaofadhiliwa na Shirika la kijerumani la Bread for the World umekutana na kuweka mikakati mbalimbali inayohusu utekelezaji. 

Kupitia warsha iliyoratibiwa na AZAKI ya Can Tanzania ,Muungano huo umekutana leo Agosti 13, 2021 mkoani  Dar es Salaam kwa ajili ya kutengeneza mkakati wa uchechemuzi na utekelezaji wa kuongeza matumizi ya huduma za hali ya hewa na nishati jadidifu kwa mamlaka na Wizara mbalimbali ndani serikali pamoja na wananchi kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo. 

Akizungumza wakati wa warsha hiyo Ofisa Mwandamizi wa Ufuatiliaji na Utathimini wa Can-Tanzania Jacquiline Masao amesema kuwa muungano huo unaundwa na AZAKI zinazojishughulisha na sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, usawa wa kijinsia, nishati jadidifu, ambazo ni sekta nyeti katika maendeleo ya jamii ya Tanzania.

"Uchechemuzi huu unategemea kuongeza matumizi ya Huduma ya hali ya hewa katika kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kama kilimo, ufugaji na uvuvi. Pia kuongeza matumizi ya nishati jadidifu kama kichocheo cha ukuwaji wa sekta nyingine na njia nafuu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,"amesema Masao.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2