MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA WIKI YA MALIKALE MIKINDANI MTWARA | Tarimo Blog


Maadhimisho ya wiki ya Malikale Mikindani yamehitimishwa rasmi na Mwenge wa Uhuru uiliokabidhiwa leo Mkoa wa Mtwara ukitokea Mkoa wa Lindi.

Akitoa ujumbe wa Mwenge kwa maelfu ya watu waliokusanyika kwenye viwanja vya Mjimkongwe Mikindani, Mkimbiza Mwenge Kitaifa CPL Rehema Ally Haji ameeleza mafanikio makubwa yaliyo tokana na maendeleo ya TEHAMA nchini yakiwemo ya urahisi wa kuhamisha taarifa za waajiriwa, uombaji wa mikopo kwa wanafunzi, uduma za afya nk.

CPL Haji, ameongeza kwa kuwataka wananchi kuchukuwa taadhari dhidi ya janga la UKIMWI kwani limekuwa likitekeza nguvu kazi ya Taifa hususan vijana pamoja na kuendelea kupambana na Janga la UVIKO 19 kama inavyo shauriwa na wataalam wa afya.

Mratibu wa Wiki ya Malikale Mikindani Bi Frida Kombe amesema Maadhimisho hayo yamekuwa na mwitikio Mkubwa wa watu na wameweza kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa majengo ya kale. 

"Mwenge wa Uhuru umetuletea Baraka katika hitimisho la Maadhimisho haya, hivyo naupongeza uongozi wa Wilaya ya Mtwara Mjini kwa  kuishirikisha  Makumbusho ya Taifa katika ratiba ya Mwenge". Alisema Bi Kombe. 

Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara yaliyozinduliwa rasmi tarehe 25 Agosti 2021 yamehitimishwa rasmi leo tarehe 28 Agosti 2021 na Mwenge wa Uhuru ambao umebeba ujumbe wa "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji".
Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani Mtwara

iongozi mbalimbali wakiwa na Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani



Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Malikale Mtwara, ambapo Mwenge wa Uhuru uliwasili kwenye viwanja hivyo vya Jengo la Kale la Soko la Watumwa Mikindani.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2