Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MASHINDANO ya Urembo 'Miss East Africa' yanatarajia kufanyika Novemba 26 mwaka huu ambapo washiriki kutoka nchi 16 wanatarajia kushiriki huku zawadi ya mshindi wa kwanza ikiwa gari mpya aina ya Nissan X Trail toleo la mwaka 2021/21 lenye thamani ya Sh.110,000,000.
Akizungumza leo Agosti 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano ya Urembo kutoka Miss East Africa Beauty Pageant Rena Callist amesema jumla ya zawadi zenye thamani ya Sh.milioni 146 zitatolewa katika mashindano hayo ya mwaka huu.
Callist amefafanua mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atazawadiwa gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000, mshindi wa pili atapata fedha Sh.milioni 11 wakati mshindi wa tatu ataibuka na kitita cha Sh.milioni tano.
Aidha kutakuwa na zawadi zingine mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zenye thamani ya Sh.milioni 20 huku akisisitiza jumla ya nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam.
Amezitaja nchi zilizothibisha kushiriki ni Tanzania,Kenya,uganda,Rwanda,Burundi, South Sudan,Ethiopia,Elitrea,Djibouti,Somalia,Malawi,Visiwa vya Seychelles,Comoros,Madagascar,Reunion na Mauritius "Calist amesema.''
Ameongeza mashindano ya Mwaka huu yanatarajiwa kurushwa moja kwa moja na kuangaliwa na watazamaji zaidi ya milioni 300 kupitia luninga na mitandao ya kijamii duniani ambapo Tanzania itafaidika na mashindano hayo moja kwa moja kwa kutangaza vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji wa biashara na utamaduni kwa ujumla.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment