Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(katikati), Kumbuka Mwakyusa kutoka Enochem Company Limited ) ambaye ni mmoja ya wadau kutoka sekta binafsi wakisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.Anayeshuhudia kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko akizungumza kabla ya utiwaji saini hati ya makubaliano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya nchini.
Sehemu ya wadau kutoka Mamlaka za Serikali wakifuatilia hotuba ya Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(hayupo pichani) Gerald Kusaya wakati wa utiwaji saini wa utiwaji saini hati ya makubaliano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya. Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya akifafanua namna ambavyo Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali pamoja na wadau wanavyoshirikiana katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya nchini.Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(kulia) na Bakari Semvue kutoka Brain Solution Ltd (kushoto) wakisaini hati hiyo ya makubaliano ya kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Florence Khambi(kushoto) akitoa maelekezo kwa mmoja wa wadau kutoka sekta binafsi namna ya kutia saini ya hati ya makubaliano ya ushirikianoKamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(katikati) na Mwenyekiti wa Tanzania Association Pharmacetical Indrustries na Mkurugenzi Mkuu wa Bahari Pharmacy Ltd Churchill Katazwa wakisaini hati hiyo ya kudhibiti kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya dawa za kulevya.Kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(katikati) Shemina Sanji kutoka Shelys Pharmaceticals Ltd ambaye pia ni Kiongozi wa TPMA wakionesha hati ya makubaliano ambayo wameisaini.Kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko.
Mwenyekiti wa Tanzania Association Pharmacetical Indrustries na Mkurugenzi Mkuu wa Bahari Pharmacy Ltd Churchill Katazwa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wadau kutoka sekta binafsi.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko(kulia) akiwa ameshika hotuba yake baada ya kutoka kuzungumza na wadau wa sekta binafsi na Mamlaka za Serkali kuhusu hati ya ushirikiano ambayo imesainiwa leo.Kushoto ni Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya akijiandaa kwenda kuzungumza na wadau hao.
Baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wakiangalia hati ya makualiano baada ya kuisani mbele ya Kamishina Jenerali wa Mamkala ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(aliyekaa katikati) , Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko (waliokaa kulia) pamoja na mmoja wa maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(kushoto) wakiwa katika picha ya pamona na wadau kutoka mamlaka za serikali na sekta binafsi baada ya utiwaji saini hati ya makubaliano kuhusu ushirikiano wa kudhibiti kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya dawa za kulevya.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa niaba ya Serikali imesaini hati ya makubaliano kati yake na Sekta binafsi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Utiwaji huo wa saini hati ya makubaliano kati ya Serikali na sekta binafsi umefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka mamlaka ya serikali na sekta hizo.
Akizungumza wakati wa utiwaji saini wa hati hiyo ya makubaliano, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuapambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya amesema kumekuwepo na wimbi jipya duniani la kutengeneza dawa mpya za kulevya kwa kutumia kemikali bashirifu na kuongezeka kwa uchepushaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Ametaja baadhi ya dawa hizo ni Fentanyl,Ketamine, Pthidine,Benzodiazenes,Tramadol na aina ya nyingine ya dawa za aina hiyo, ambazo hutumika kama dawa za haramu za kulevya,hivyo ushiriakiano kati ya Serikali na sekta binafsi ni muhimu katika kukabiliana na na changamoto hiyo.
"Kama mtakumbuka kati ya miaka ya2015 na 2017 tulikuwa na changamoto ya usafirishaji haramu wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya ambapo nchi yetu ilitumika kama kituo cha kusafirisha bidhaa hizo kutoka nchi za Asia kuja Tanzania na kisha kupelekwa nchi nyingine.
"Hata hivyo kazi kubwa iliyofanywa na Mamlaka za Serikali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ,wadau kutoka sekta binafsi na kwa kushirikiana na bodi ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya Tanzania tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti uhalifu huo, "amesema.
Amefafanua mafanikio hayo yaliipa Tanzania sifa kuwa mwenyeji mkutano wa kujadili ushirikishwaji wa sekta binafsi Oktoba mwaka 2019 jijini Dar es Salaam chini ya uratibu na bodi ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya(INCB).
Ameongeza mojawapo ya maazimio yalikuwa ni kwa nchi ya Tanzania kutambuliwa kuwa ya mfano kwenye ukanda huu kutokana na mafanikio yaliyofikiwa katika kudhibiti kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya .Pia Tanzania ilipewa jukumu la la kuelimisha na kuhamasisha nchi nyingine katika ukanda huo namna bora ya udhibiti wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Hivyo amesema ili kuendelea kukabiliana na changamoto ya uchepushaji huo, Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali ambazo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA),Bohari Kuu ya Dawa(MSD),Baraza la Famasia (PC) pamoja na sekta binafsi wanatekeleza mradi wa pamoja chini ya bodi ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya.
Kamishina Jenerali Kusaya amesisitiza anatambua ushiriki wa wadau hao katika kuandaa nyaraka za mkataba huo wa hiyari wa ushirikiano.Hivyo leo tumekutana kwa ajili ya utiaji saini hati ya makubaliano ya ushirikishaji sekta binafsi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu.
"Mkataba huu utaanza na kampuni takribani 32 na vyama viwili vya wadau wanaojishughulisha na dawa tiba zenye asili ya kulevya ambavyo i TPMA na TAPI zinazowakilisha kampuni zinazofanya kazi hizo,"amefafanua wakati akielezea umuhimu wa hati hiyo ya makubaliano.
Awali Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko amefafanua kemikali bashirifu ni kemikali zenye kuhitajika kwa matumizi ya kawaida katika shughuli za kila siku.Aidha kemikali hizo zinaweza kuchepushwa na kutumika kwa malengo yasiyokusudiwa ikiwemo kutengeneza dawa za kulevya , mfano kemikali hizo ni Potassium Permanganate ambazo zinatumika kwenye viwanda vya nguo.
Pia Sulphuric Acid, Toluene, Acetone na Chloroform ambazo zinamatumizi mbalimbali kwenye viwanda na maabara."Ili kuzuia hali hiyo isitokee na kuwa na mfumo madhubuti Serikali imetunga na kupitisha sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali.
"Pamoja na uwepo wa sheria na matakwa yake leo hii hatua nyingine tena ambapo Mamlaka za Serikali na sekta binafsi tumeweka historia ya kusaini makubaliano ya hiyari ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.Ni matarajio yetu makubaliano haya yatakuwa chachu ya kupeana taarifa zitakazowezesha kuzuia na kudhibiti uchepushaji huo,"amesema Dk.Mafumiko.
Aidha amesema Mamlaka anayoiongoza na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba zina majukumu ya kusimamia kemikali bashirifu zote za viwandani na majumbani na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika matumizi yake yaayokubalika.
"Jukumu la uchepushaji wa kemikali bashirifu liko mikononi mwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya , kwa kuzingatia utaratibu huo mkataba wa hiyari uliosainiwa leo unakwenda kupanua wigo wa mapambano kwa niaba ya mamkaka zote za serikali pamoja na sekta binafsi,"amesisitiza Dk.Mafumiko.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment