Mwanariadha wa zamani na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Mbio za Ocean City Community Kanali Juma Ikangaa akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yatakayofanyika Oktoba 3 mwaka huu.
Mwakilishi kutoka Jan International Basilisa Biseko akizungumzia ushiriki wa kampuni yao katika mashindano hayo ambayo leo wametiliana saini makubaliano ya zawadi ya gari kwa washindi wa upande wa wanaume na wanawake kwenye mbio za Ocean City Community zitakazofanyika Oktoba 3 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Jan International Muhamad Chishti (katikati), Mwenyekiti wa Riadha Dar es Salaam Catherine Nyamko, Mwakilishi kutoka One Plus Event Bakari Ramadhan (wa kwanza kushoto) , mwanariadha wa zamani Kanali Juma Ikangaa (wa pili kulia) wakikata utepe kuashirikia uzinduzii wa Mashindano ya Ocean City Community Marathon zitakazohusisha Mbio za Km 21.1, km 10 na Km 5 na Zitafanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja ya The Green Oysterbay.
Mkurugenzi wa Jan International Muhamad Chishti (kulia) na Mwakilishi kutoka One Plus Event Bakari Ramadhan wakitia saini makubaliano ya zawadi ya gari kwa washindi wa Ocean City Community Marathon zonazotarajiwa kufanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja ya The Green Oysterbay.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
WANARIADHA nchini wametakiwa kuongeza juhudi,kujituma na kufanya mazoezi ili waweze kuiwakiliasha nchi kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.
Hayo yanesemwa na Mwanariadha wa zamani Kanali Juma Ikangaa wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya zawadi ya magari ya washindi wa Mbio za Ocean City Community kati ya Kampuni ya One Plus na Jan International yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Kanali Ikangaa amesema, ili taifa la Tanzania liweze kufika mbali katika mchezo wa riadha haina budi kwa wanariadha kufanya mazoezi kwa bidii zote ili wapate nafasi ya kuwa wawakilishia wa mashindano makubwa ikiwemo Jumuiya madola, Olimpiki na kurudi na medali.
“Kwanza nimefurahi kuona zawadi ya gari kwa upande wa Wanawake na upande wa wanaume ambapo zitakabidhiwa kwa wale watakaoshinda kwenye mbio za Km 21.1 na cha ziada ni kuwa fedha zitakazopatikana zitaenda kwa watoto yatima 200 ambao watatengenezewa bima za afya,” amesema
Kwa upande wa Mwakilishi kutoka Jan International Basilisa Biseko amesema mbio Katika kuhakikisha michezo inaendelea hapa nchini, kampuni ya Plus one imeweza kuandaa mashindano ya riadha, yakiwa na lengo kuu la kukusanya kiasi cha fedha kuweza kusaidia Watoto yatima takribani 200 kupatiwa huduma ya bima ya Afya.
Biseko amesema wao kama Jan International waliweza kupokea maombi kutoka One Plus ya kuweza kuwa moja ya wadhamini na walilipokea hilo kwa mikono miwili kwa sababu linahusisha jamii.
“Jan tumetoa magari mawili aina ya Passo na tutayakabidhi kwa washindi wa mbio za Km 21.1. na tumefurahia sana ushirikiano huu kwani tunaamini huu ni mwanzo kikubwa tutaendelea kusaidia jamii kwa njia mbalimbali’l amesema Biseko.
“Kampuni ya Jan International inafuraha sana juu ya ushirikiano huu, na inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa waandaaji, na jamii kwa ujumla , ikiwa pia ni mpango mkakati wa kampuni katika kurudisha kwa jamii ambayo ndio wateja wetu,”
Naye Bakari Ramadhan mwakilishi kutoka Plus One amesema Kampuni ya Plus one inajihusisha na uaandaaji wa matukio, imeeleza kuwa ni jukumu la kila mwanajamii kufanya jambo kwa jamii yake, na ndio sababu kuu iliyopelekea wao kuja na wazo la kuandaa mashindano haya ya riadha.
Amesema, mashindano hayo ya Ocean City Community Marathon yatahusisha wakimbiaji na wanariadha na yatafanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Viwanja vya The Green Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
“Mbio zetu tumeziboresha na kwa washiriki wote ikitokea umeshinda na umegundulika umetumia dawa za kuongeza nguvu hatuna budi kukunyang’anya zawadi uliyopatiwa na pia tutakuwa na zawadi kwa washindi wa pili hadi wa kiume kwa upande wa wanaume na wanawake,” amesema
Ramadhan amesema,” fedha zitakazopatikana zitaenda kuhudumia watoto yatima 200 ili kuwakatia huduma ya bima ya afya na huu ni mwanzo tutaendelea kuboresha kila tutakapokuwa tunaandaa mashindano mengine”
Mashindano hayo yatahusisha mbio za umbali wa Km 21.2, Km 10 na Km 5 na zitafanyika Oktoba 3 mwaka huu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment