RAIS SAMIA SULUHU AKOSHWA NA JITIHADA ZA BENKI YA NBC KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU ZANZIBAR | Tarimo Blog

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahia  pamoja na baadhi ya  viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua  Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Pamoja nae ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui (wa pili kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman (Kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke  (Kushoto).

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  akijadili jambo na baadhi ya  viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua  Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  wakati Rais alipokuwa akigagua jengo la madarasa ya Skuli ya  Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Monekano wa jengo la madarasa ya Skuli ya  Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (Kulia) akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  zawadi kwa niaba ya Umoja wa wanawake wa benki hiyo ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kutambua jitihada za Rais Samia katika kuliongoza taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahia  pamoja na baadhi ya  viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua jengo la madarasa ya Skuli ya  Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa Skuli ya  Maandalizi ya Kizimkazi (Kushoto) wakati akijiandaa kuzindua jengo la madarasa ya skuli hiyo yaliyojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Wengine ni pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia)

Baadhi ya wagenini waalikwa pamoja viongozi wa benki ya NBC wakifuatilia makabidhiano hayo.

Wanafunzi na wakazi wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakiwa wameketi pembeni ya Kliniki inayotembea (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar

Wanafunzi wa Skuli ya  Maandalizi ya Kizimkazi wakitoa burudani mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.


 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2