Ubalozi unapenda kuwajulisha kuwa Serikali ya Oman imeondoa katazo la kuingia Oman kwa abiria kutoka Tanzania na nchi zingine zilizokuwa kwenye kundi hili.
Hivyo basi kuanzia tarehe 1 September 2021 Abiria wanaopandia ndege zao Tanzania kuja Oman wataruhusiwa kuingia Oman kwa kutimiza masharti yafuatayo:
- 1. Kuwa na cheti cha chanjo ya Uvika 19 (COVID 19) kinachothibitisha kuwa abiria
amekamilisha dozi mbili za chanjo au dozi moja ya chanjo kwa zile ambazo dozi ni moja chanjo iwe imefanyika sio chini ya siku 14 kabla ya tarehe ya kuingia Oman
- 2. Cheti cha chanjo ni lazima kiwe na alama ya QR (QR Code)
- 3. Chanjo iliyotumika ni lazima iwe miongoni mwa chanjo zilizoidhinishwa kutumika nchini
Oman
- 4. Chanjo zilizoidhinishwa Oman ni Johnson and Johnson, AstraZeneca-Oxford,
AstraZeneca-Covishield, Pfizer ,Sinopharm, Sirovac, Sputnik na Moderna
- 5. Cheti cha kupima Uvika 19 kinachoonyesha kutokuwa na maambukizi (Negative PCR
Test Certificate ), vipimo vifanyike masaa 72 kabla ya safari
Pamoja na kuwa suala la chanjo linabaki kuwa hiari ya mtu binafsi, lakini ni muhimu kufahamu kuwa hlari hii inakoma pale tu masharti, maelekezo na ya umma (public health) katika nchi mnayoishi zinapoelekeza vinginevyo au masharti ya mwajiri wako yanapoelekeza vinginevyo
kwa hali hii mnatakiwa kuzingatia kuwa serikali ya Oman imetoa maelekezo kuwa kuanzia tarehe 1 septemba 2021 wale wote wanaoingia kwenye maeneo ya umma na yenye mikusanyiko ya watu (PUBLIC PLACES) kama vile maofisi, maduka makubwa, hospital, usafiri wa umma na viwanja vya ndege ni lazima wawe na vyeti vya kuonyesha wamepata na kukamilisha chanjo ya uviko 19
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment