NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AZINDUA PROGRAMU YA MAFUNZO YA URASIMISHAJI BODABODA, BAJAJI | Tarimo Blog

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi (wa pili kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Urasimishaji Biashara ya Bodoboda na Bajaji  ulioandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwenye Uwanja wa  Jamhuri jijini Dodoma leo Agosti 27, 2021. Kutoka kulia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri na Jane Lyimo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa MKURABITA.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi (wa pili kushoto) akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Urasimishaji Biashara ya Bodoboda na Bajaji. 
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Kasyenene akielezea kuhusu umuhimu wa programu hiyo wakati wa uzinduzi ambapo amesema kuwa inaanza jumatatu katika Kata 40 za Dodoma Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri akizungumza katika hafla hiyo ambapo amesisitiza umuhimu wa Bodaboda na waendesha Bajaji kupata mafunzo ya usalama barabarani.
Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akiipongeza MKURABITA  kuanzisha mafunzo hayo katika jimbo hilo na kwamba yatawanufaisha vijana wengi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Meja mstaafu Risasi akisisitiza suala usafi wa kimwili na kimavazi kwa waendesha bodaboda/bajaji wanapokuwa kazini.
Diwani wa Kata ya Mihuji, Dodoma, Beatrice Ngerangera akiishukuru Mkurabita kuanzisha mafunzo hayo na kuahidi kutoa ushirikiano.
Naibu Waziri Ndejembi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Biashara wa MKURABITA, Jane Lyimo.
Meneja Urasimishaji Biashara wa MKURABITA, Harvey Kombe akisalimiana na Naibu Waziri Ndejembi.
Naibu Waziri Ndejembi akipata maelezo katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jinsi itakavyoshiriki kutoa mafunzo ya jinsi ya waendesha Bodaboda/ Bajaji kupata leseni ya udereva.
Naibu Waziri Ndejembi akiwa Banda la Benki ya CRDB akipata maelezo kuhusu utaratibu wa kuwapatia mikopo waendesha Bodaboda/Bajaji.
Naibu Waziri Ndejembi akijadiliana jambo na viongozi wa MKURABITA.


Baadhi ya viongozi wa MKURABITA wakiwa pamoja na waendesha Bodoboda na Bajaji mkoa wa Dodoma wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya viongozi wa MKURABITA wakiwa katika shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dodoma akiupongeza uongozi wa MKURABITA kwa kuanzisha mafunzo hayo kwa wanachama wao wa kada mbalimbali na kwamba wako tayari kushirikiana nao.
Kikundi cha ngoma cha Nyati kutoka Chamwino kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu  baada ya uzinduzi kumalizika.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Deogratius Ndejembi amezindua Programu ya Mafunzo kwa wafanyabiashara wa Bodaboda na Bajaji Jijini Dodoma.

Akizindua programu hiyo, Ndejembi ameupongeza uongozi wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABIKA) kuanzisha mafunzo hayo ya kurasimisha biashara hizo kwa lengo la kuaminika na taasisi za fedha ili wapatiwe mikopo na kuweza kumiliki vyombo hivyo vya usafiri.

Ndejembi ametoa wito kwa vijana waendesha bodaboda kujitokeza kwa wingi wakati wa mafunzo hayo katika kata zao na kuwapa taarifa wenzao kuhusu umuhimu wa maafunzo hayo.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Kasyenene amemshukuru, Naibu Waziri Ndejembi kuzindua programu hiyo ambayo mafunzo yanatarajiwa kuanza Jumatatu katika Kata 40 za Dodoma Mjini  na kushirikisha zaidi ya waendesha bodaboda/ bajaji 2500 wanawake kwa wanaume.

 
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue kilichozungumzwa na Naibu Waziri, Ndejembi, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabiri Shekimweri na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja mstaafu Risasi.... 
Attachments area
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2