RAIA wa Misri, Mohamed Shalabi, Ally Rajabu na Shebet Benson raia wa Uganda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya usafirisha haramu wa binadamu.
Katika ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Godfrey Ngwijo kutoka idara ya Uhamiaji
mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya imedai, Agosti 4, 2021 huko katika hoteli ya Avone iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Shaban akiwa ni raia wa Misri na Mauritania alikutwa akisafirisha jumla ya watu 95.
Imedaiwa kati ya watu hao 90 ni Watanzania na watano raia wa burundi.
Katika shtala la pili imedaiwa siku hiyo katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam mshtakiwa Rajabu akiwa raia wa Tanzania alikutwa akiandaa mpango wa wa kusafirisha watu hao 95 kwa kuwapatia mafunzo kwa lengo la kuwasafirisha kwenda Canada na Mauritania.
Imeendelea kudaiwa kuwa, siku hiyo huko katika hospitali ya Kimataifa ya Sali iliyopo Masaki katika Wilaya ya kinondoni mshtakiwa Shebet alikutwa akifanya kazi ya kitaaluma bila ya kuwa na kibali.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo dhidi ya washtakiwa Mohamed na Shebet umekamilika.
Hata hivyo mshtakiwa Rajabu amekiri kutenda kosa hilo.
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa Shaban alidai kuwa yeye alikuja Tanzania kwa mualiko wa mtu aliyemtaja kwa jina moja la Rahma kwa ajili ya kuja kufanya biashara ndogo na alipofika aliwauliza kuhusu kibali, ambapo alitakiwa kulipa USD 2500 ambazo amedai alilipa.
Amedai lakini kabla hajapata vibali alikamatwa, na huyo Rahma hana ofisi na wakati yeye anakamtwa alikuwa nyumbani kwa huyo mwanamke.
Hata hivyo Hakimu Isaya alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kwa sasa siyo muda sahihi wa kueleza hayo yote kwani ndio kwanza kesi inaanza na ukifika wakati utaieleza mahakama.
Aidha mahakama imesema dhamana ipo wazi kea washtakiwa ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika, mmoja awe ni muajiriwa wa Taasisi yoyote inayotambulika lakini mshtakiwa Shebet na Shaba ambao siyo raia wa Tanzania wanatakiwa kuwa na wadhamini watatu raia wa Tanzania na pia wawasilishe hati zao zao za kusafiria na hawatatakiwa kutoka nje ya Tanzania.
Kesi hiyo itaendelea kesho Agosti 11, 2021
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment