Na Atley Kuni - KAHAMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu, amezitaka Halmashauri 11 nchini kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndani siku 14, ni kwa nini wametekeleza mpango wa Lishe kwa kiwango cha asilimia 25.
Waziri Ummy ametoa maaagizo hayo, leo Agosti, 26, 2021, wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Kupitia Afua za Lishe, unaofanyika mkoani Shinyanga katika Manipaa ya Kahama, ambapo amesema lengo la Serikali nikuona nchi inaondokana na suala la uatapiamlo na udumavu wananchi wake
“Nizitake Halmashauri za Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Halmashauri Wilaya Buhigwe mkoani Kigoma, Halmashauri ya Handeni Mji mkoani Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, Halmashauri ya Manispaa Shinyanga mkoani Shinyanga, Halmashauri Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora mkoani Tabora, Halmashauri Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya na Halmashauri Wilaya ya Itigi mkoani Singida zitoe maelezo kwa katibu Mkuu TAMISEMI ndani ya Siku 14” Alizitaja Waziri Ummy.
Mbali na maelekezo hayo, Waziri Ummy hakusita kuwapongeze sana Wakuu wa Mikoa kwa kuhakikisha ongezeko la utoaji ya fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe, kutoka asilimia 22 kwa mwaka wa fedha 2017/18, asilimia 52 kwa mwaka wa fedha 2019/20 na kufikia asilimia 57 kwa mwaka wa fedha 2020/21.
Ongezeko hilo la utoaji wa fedha amelitaja kama kuwa ni mabadiliko chanya katika kutekeleza afua zingine zinazotegemea kiashiria cha kupanga na kutumia fedha katika Halmashauri, huku akiataka kuongezwa juhudi zaidi ili kukidhi kile walichokubaliana cha shilingi 1000 kwa kila mtoto chini ya miaka itano.
Awali akitoa maelezo ya utangulizi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe alieleza chimbuko na maudhui ya Mkataba huo wa Lishe ni Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, aliyepewa dhamana ya kuisaini mkataba kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan mwaka 2017, akiwa Makamu wa Rais ambapo katika muktadha huohuo alielekeza kuendelea kusaini mikataba husika hadi ngazi ya kijiji/Kata na mitaa yote nchini.
Kikao cha hicho cha Mwaka cha tathmini ya tano ya lishe kinafanyiaka katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanya.
Mkurugenzi wa Geita Mji, Zahara Michuzi akipokea cheti kutoka kwa Mhe. Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi mara baada ya Halmashauri hiyo kuwa miongoni mwa Halmashauri vinara kwenye Lishe.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera, akipokea cheti cha Ushindi wa kwanza katika kushughulikia afua za Lishe.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, akitoa neon la utangulizi wakati wa kikao hicho.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment