Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WASANII wa Zenjifleva kutoka visiwa vya karafu Zanzibar wameaswa kutotumia vilevi wawapo katika Matamasha ya kimuziki kwani vinawapumbaza na kupelekea baadhi yao kufanya vitendo vya kukiuka maadili
Akizungumza na Michuzi Tv Msanii wa zenjifleva ambae pia ni Balozi wa Sanaa kutoka visiwa vya Zanzibar Mustafa yussuf maarufu kama "Smile the genius" ambae anavuma kwa Sasa na albam yake ya "Marashi ya karafuu" ameeleza kwa namna gani anachukizwa na baadhi ya wasanii hao kutumia vilevi katika majukwaa ya Burudani na kutolea mfano mojawapo ya Tamasha ambalo ameona wasanii wakitumia vilevi hivyo.
"Wengi wanaotumia vilevi huwa hawajiamini katika kazi zao naamini kwenye kipaji Wala hakitumii nguvu nyingi kama jinsi wanavyotafsiriwa Miongoni mwa watu hivyo basi kitendo hicho niliweza kushuhudia Hilo."
Kwa upande wake ameeleza siri ya yeye kufanya vizuri kazi zake za Sanaa ni pamoja na kufanya Mazoezi huku swala la maji mengi Ikiwa ni kilevi chake.
Hata hivyo Smile ameweka bayana Kuwa kupitia Tamasha la zuchu vipi vingi ambavyo amejifunza kubwa ni kwa jinsi gani anaweza kusimama mwenyewe katika kazi zake na kwa namna gani anaweza kuandaa show zake
.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment