Raisa Said,Bumbuli
WAKUU wa Wilaya za Korogwe na Lushoto wamechukua hatua kadhaa kuzima mgogoro wa ardhi uliokuwa unafukuta katika kijiji cha Kwebamba katika maeneo ambayo yanasemekana yamegunduliwa madini aina ya silicon.
Wakuu hao, Kalisti Lazaro wa Lushoto na Basila Mwanukuzi wa Korogwe walitoa maamuzi hayo baada yakikao cha Ujirani mwema kilichofanyika katika Kitongoji cha Kwebamba,lilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli kufuatia taarifa za wananchi kumtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kuingilia kati mgogoro wa ardhi unazingonganisha Halmashauri mbili za mkoa wa Tanga juu ya umiliki wa eneo ambalo linasemekana limegunduliwa madini ya aina ya silicon.
Akitangaza maamuzi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto alisisitiza kuwa wakuu wa wilaya hawakwenda kubadilisha mipaka kwa mujibu wa Tangazo la serikali.
“Sisi kama wakuu wa Wilaya tumekuja kufanya maamuzi ili muendelee kuishi kwa amani. Kila kitu kina mamlaka yake. Sasa haya ya serikali, wakurugenzi na wakuu wa idara na Halmashauri zote mbili za wilaya watakaa vikao kuzungumzia suala hilo na kufanya mapendekezo, kama watabadilisha GN kwa vikao halali au watabdilisha ramani hiyo ni kazi ya wataalamu,” alisema.
Alisema kuwa wameamua shughuli za kiutawala za kijiji hicho ziendelee kama ioivyolues chini ya Halmashauri ya Bumbuli hadi hapo hatua za kubadilisha Tangazo la serikali la Mwaka 1963 lililounda mipaka ya wilaya zitakapochukuliwa.
Tangazo hilo kwa mujibu wa Lazaro liliweka eneo hilo katika wilaya ya Korogwe wakati ambapo ramani inaonyesha liko katika wilaya ya Lushoto
“sisi kama viongozi tumetumia busara ifuatayo vingozi wa Bumba na wananchi wa kijiji hicho na vitongoji vyake, kwa sasa, wanabaki kama ilivyokuwa kwa mujibu wa uchaguzi ulivyofanyika. Hatuwezi kubadilisha sasa hivi. Vijiji kama vijiji ni halali kwenye usajili, mgogoro uko katika Tangazo la Mwaka 1963 na mwaka 1948,” alisema.
Alisena kuwa kinachowagonganisha vijiji vyote ni ugawaji wa mapori, ugawaji wa msitu na madini. Alipiga marufuku kwa serikali za kijiji kujihusisha na ugawaji wa vitalu vya uchimbaji. “Suala la ugawaji wa vitalu vya kuchimba madini wa utoaji wa vibali ni mamlaka husika ambayo ni Ofisi ya Madini,” alisema.
Alifafanua kuwa kazi ya Halmashauri husika ni kusimamia namna ya uchimbaji sio kugawa wala kitoa leseni. “Eneo likishakuwa na maliasili kijiji hakina mamlak. Suala kugawa eneo la machimbo,na kutoa leseni ni mamlaka husika ambao ni Ofisi ya Madini ya Mkoa,” alisema.
Akizungumzia kuhusu ugawaji wa maeneo ya pori ambayo ambayo hayawana watu inabidi serikali za kijiji ziwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji. Alisema ana taarifa kuwa vijiji husika, Mtoni Bombo na Bumba havina mipamgo hiyo.
“Hivyo kuanza sasa hivi hakuna kijiji kinaruhusiwa kukaa kikao na kugawa ardhi au kuuza ardhi na kuchukua ushuru hadi hapo Mamlaka za Halmashauri za vijiji husika zitakapowasilisha mpango huo katika muda wa siku 60 kuonyesha matumizi mbalimbali. Mkiendelea kugawa na kuuza na kuchukua shilingi elfu tano tano mtaleta vita kwenye vijiji vyetu.” Alisisitiza.
Lazaro alifafanua kuwa eneo la msitu siyo mali ya vijiji, bali mali ya Wakala wa Misitu (TFS), hivyo ni marufuku serikali za vijiji kukaa na kugawa maeneo hayo kwa sababu maeneo hayo siyo ya kijiji chochote.
Alisema wameelekeza TFS wasimamie na walinde maeneo yao yasivamiwe. Kama wameona hayafai tena kuwa msitu watoe taarifa na kukabidjhi kwa mamlaka husika ili lipangiwe matumizi na sio serikali za kijiji kugawa na hiyo ndiyo inaleta matatizo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi alisisitiza kuwa wao kama viongozi lengo lao ni kutenda haki lakini lazima Tanzania inaongozwa na sheria ambazo zitawafanya wafanye maamuzi sahihi.
“Tumekaa muda mrefu. Tumejadiliana, tumeshirikishana na wataalamu wa ardhi, tumeangalia ramani, kila kitu tumeangalia, tumejadiliana kwa kina, tumeshauriana ili tufanye maamuzi yaliyo sahihi kwa ajili ya wananchi wetu wote,” alisema.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Tanga, Shaabani Mruma, alisema mgogoro ulishawahi kushughulikiwa miaka ya nyuma (2007) na Wizara ya Ardhi waishirikiana na Wilaya hizo mbili.
Alisema walianza kuushughulikia mwaka 2018 na kimsingi waliangalia matangazo yaliyounda wilaya hizo mbili na Halmashauri ya Bumbuli na kimsingi matangazo yote ni halali kisheria.
Mruma alisema walifika katika eneo husika walibaini kuwa kuna vijiji 4 ambavyo vinaingia katika mgogoro ambavyo ni Kikumbi, Bumba, Kalalani na Mtoni Bombo
Hata hivyo, alieleza kuwa vyote vimesajiliwa na Tamisemi lakini vilivyopimwa ni viwili, Mtoni Bombo na Kalalani na vingine havijapimwa. “Inawezekana havikupimwa makusudi pengine kutokana na mwingiliano wa matangazo ya serikali,” alieleza.
Alisema kuwa kijiji cha Mtoni Bombo hakina matatizo kiko ndani ya mipaka ya wilaya ya Korogwe. Kijiji Bumba, kwa mujibu wa Tangazo la serikali kipo ndani ya mipaka ya Korogwe lakini huduma zake zote kinapata kutoka Bumbuli kwa maana ya elimu, afya na masuala ya uchaguzi.
Mruma alisema kuwa walichobaini ni kuwa kulikuwa na migogoro inahusu ardhi wakigombea ugawaji wa ardhi katika maeneo hayo. Kila kijiji kilikuwa kinadai haki ya kugawa ardhi.
Pia alisema kuwa walibaini kuwa Tangazo la Halmashauri halikuzingatia mipaka mama ya Wilaya ya Lushoto.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment