Na Angela Msimbira TAMISEMI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriakli za Mitaa Dkt. Festo Dugange amewataka Waratibu wa Maabara wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanathibiti upotevu wa bidhaa za afya na kusimamia upotevu wa fedha zinazotokana na utoaji wa huduma za maabara nchini ili zitumike kwenda kununua vitendanishi.
Akifungua kikao kazi cha waratibu wa maabara wa Mikoa na Halmashauri leo Mkoani Dodoma Dkt. Dugange amesema katika eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa mapinduzi makubwa ni kuboresha upatikanaji na matumizi sahihi ya bidhaa za afya vikiwemo vitendanishi vya maabara.
Anafafanua kuwa idadi ya vitendanishi vya maabara hailingani na idadi ya wagonjwa waliohudumiwa katika vituo vya kutolea huduma jambo ambalo halileti picha nzuri, kwa kuwa maeneo mengi idadi ya vitendanishi na wahudumiwa bado ni changamoto.
Amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia kwa karibu na kuhakikisha kila bidhaa ya afya inatumika kwa kufuata miongozo na ufanisi unaoendana na mahitaji ambayo yanatakiwa kuonekana katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Aidha,Dkt. Dugange amewaagiza wataalam wa maabara kuhakikisha wanaratibu mapato yanayochagiwa katika sekta ya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini, ni wajibu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment