RC DAR AMWAMBIA RAIS MKOA UKO SALAMA,MEYA KINONDONI AANIKA MABILIONI YALIYOKWENDA KAWE | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe, Michuzi TV


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kwamba mkoa huo uko shwari,uko salama na shughuli za maendeleo zinaendelea.

Akizungumza leo mbele ya Rais Samia , Makala amesema mkoa uko shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao, huku akifafanua ameanzisha utaratibu wa kupita jimbo kwa jimbo na Ijumaa alikuwa katika ziara ya kukagua mradi mkubwa wa maji ambapo Serikali imetoa fedha Sh. 65 kuwasaidia wananchi katika jimbo la Kawe.

"Nimefanya  ziara katika maeneo mbalimbali ya Kawe na niseme mbele ya wananchi wa Tegeta watapata  maji ya uhakika.Jumatatu nilikuwa nasikiliza kero kutoka Kata zote lakini pamoja na kusikiliza kubwa ambalo wameniomba ni kutatua changomoto ya mafuriko ya wananchi kuanzia Namanga basi haya wanaosumbuliwa wakati wa mvua.

"Lakini kama ulivyosema utatimiza ahadi zote zilizoachwa na Awamu ya Tano wananchi waliahidiwa lakini tukagundua hapa Namanga walikuwa hawajafanyiwa usanifu , watalamu sasa wamekamilisha kazi na mafuruko yatabaki kuwa historia, ramani ninazo , hayo ni maelekezo yako kuona tunatatua kero za wananchi.

"Lingine ni kwamba wanakushukuru kwa kazi kubwa , hapa Tegeta wameshapokea fedha Sh.bilioni tano kujenga soko , pia ipo habari ya kuboresha stendi yao, hivyo miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea.Niwahakikishie wananchi hawa wanakupenda na ndio maana wamejitokeza kwa aendelea."

Kwa upande wake Meya wa Kinondoni Songoro Mnyonge amesema kazi ya kusimamia Ilani ya CCM inaendelea ili kuhakikisha huduma za jamii zinaendelea kuboreshwa."Tumehakikisha hospitali yetu ya Wilaya iliyopo Mabwepande inakamilika mwaka jana ulikuja kuweka jiwe la msingi hospitali ile imekamilika na imebaki kuzinduliwa tu na kwa kuwa Mkuu wa Mkoa amekuomba uje kufanya ziara kwenye mkoa wetu tunakuomba uje uizindue.

"Pamoja na hilo tunaomba kukushukuru kwani licha  kuwa na hospitali ya Wilaya ndani ya Mabwepande tumehakikisha tunakuwa na zahanati katika kila kata katika jimbo la Kawe , hivyo kote huko kuna Zahanati, lakini pia umetulitea Sh.bilioni 1.5 tuongeze vituo vya afya vitatu ndani ya jimbo la Kawe ili wananchi waweze kuishi vizuri,"amesema.

Ameongeza kwenye miundombinu, TARURA wamepewa Sh.bilioni 14 kwa ajili ya barabara za jimbo la Kawe."Nami niongeze kukushukuru mbali ya hizo fedha umetuletea tena Sh.bilioni 234 kupitia mradi wa Maendeleo ya Kuendeleza Dar es Salaam zinakuja ndani Kawe ,kupitia fedha hizo kilometa 80 lami zitatandazwa."



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2