Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
BONDIA Juma Chocki amesema hakuna siri kubwa ya ushindi zaidi ya kufanya mazoezi, kutumia akili, mbinu na kufuata kile unachofundishwa na kocha wako uwapo mazoezini na hata ulingoni.
Choki katika pambano lake alipigana na Bondia kutoka Zambia ‘MDF’ Salim Chamaza na kumshinda kwa Knockout katika raundi ya tatu ya pambano hilo.
Amesema, sasa anaendelea kujifua zaidi ili apate mapambano makubwa na ya kimataifa na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwakilisha nchini.
“Siri kubwa ya ushindi ni mazoezi, nimekuwa nafanya sana mazoezi na ili niwadhihirishie watanzania kuwa mimi ndio King of the Ring lazima nipate ushindi kwenye kila pambano,” amesema
Choki amesema, hili ni pambano lake kubwa la kwanza na la tano toka aanze kucheza ngumi za ushindani na anamshukuru mungu kwa kumuwezesha kushinda kwa KO tena raundi ya tatu.
“Unajua mm hili ndio pambano langu la tano toka nianz kucheza ngumi za kulipwa na mpinzani wake ameshacheza mapambano mengi na uwezo wake ni mkubwa ila namshukuru mungu nimepeweza kupambana na kumpiga kwa KO,”
Choki amewashukuru watanzania kwa sapoti kubwa na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika kila pambano atakalocheza.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment