CHONGOLO AWAPONGEZA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) | Tarimo Blog


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewapogeza Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanachama wapya, kuhimiza wanachama kulipa ada na kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  lililofanyika leo tarehe 20 Disemba, 2021 Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Maeneo hayo matatu kwa CCM ni muhimu sana, bila hayo hakuna Chama wala Jumuiya, kwani bila kuingiza wanachama wapya maana yake waliopo wataendelea kupungua, bila kuwa na msingi imara wa uchumi jumuiya itakuwa ombaomba na bila kujenga uhai wa jumuiya hatutakuwa na jumuiya imara na yenye nguvu ya kusimamia maslahi ya wanawake nchini.

Aidha, UWT kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa Ndg. Gaudensia Kabaka, imetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda kamati maalum ya kumshauri kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia, ambapo itasaidia katika kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika fursa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Uwt Zanzibar Ndg. Thuwaiba Kisasi amesisitiza kuwa, wanawake wataendelea kusimama kidete katika kusimamia maslahi ya wanawake wote nchini na ya Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho za kawaida, kimehudhuriwa pia na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo Katibu wa NEC, Oganaizesheni Ndg. Maudline Castico na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dkt. Edmund Mndolwa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuongoza katika miradi ya kiuchumi Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Ndugu Yasmin Bachu (kushoto) leo Makao Makuu ya CCM, Dododma. (Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akifafanua jambo katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  lililofanyika leo tarehe 20 Disemba, 2021 Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Makao Makuu ya CCM Dodoma. (Picha na CCM Makao Makuu)

Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndugu Thuwaiba Kisasi akihutubia wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma. (Picha na CCM Makao Makuu)
Mwenyekiti wa UWT Ndugu Gaudensia Kabaka akihutubia wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Makao Makuu ya CCM Dodoma. (Picha na CCM Makao Makuu).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2