Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mjini Dodoma, alipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera akitoa taarifa ya maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe Jenista Mhagama ( katikati) akipata maelezo alipokuwa akikagua jengo la kutangazia Matokeo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi amabalo limekamilika kwa 97%
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akikagua Samani mbalimbali katika moja ya Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mjini Dodoma.
…………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Taasisi huru ambayo imewekwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Taasisi hii inategemewa katika kuhakikisha ustawi wa Taifa unaendelea kuwepo, kwa kuendelea kufuata sheria, taratibu na kuwa wazalendo na waaminifu kwa Taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu alipotembelea Ofisi za Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma 20/12/21/ kukagua maendeleo ya ujenzi na kuzungumza na watumishi wa Ofisi za Taasisi hiyo . Ameeleza kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi inategemewa na Taifa zima, kubaki katika ustawi tulionao na hasa katika kutunza Amani na Utulivu Mshikamano na Umoja ambao umekuwepo katika taifa hili ndani ya miaka 60 ya uhuru na tangu tumeanza kufanya chaguzi zetu.
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ulisaidia Serikali kuja na aina ya michoro itakayoendana na aina ya ardhi iliyopo Dodoma. Lakini kujenga jengo linaloendana na thamani halisi ya fedha (value for money) ikaonekana, mpaka kuelekea kumaliza ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Uchaguzi limegaharimu kiasi cha shilingi Billioni 21. Waziri Mhagama amewapongeza wakandarasi wa SumaJKT na ARU Consultant kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi. Ameendelea kuwahimiza TBA Wakala wa Majengo, kusimamia vizuri kwa kushirikiana na ARU na SumaJkt ili kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza katika mradi yanarekebishwa.
Amefafanua kwamba wakati wa kupigania Uhuru Sera na mitizamo yote ya Kiutawala na Kiutendaji na Kisiasa na Demokrasia ilikuwa ni kuhakikisha tunapata Uhuru. Lakini sasa baada ya kupata Uhuru ni lazima tuhusianishe kila jambo na maendeleo ya Nchi. Ameongeza kusema Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kutekeleza kazi zake, hivyo hivyo mwelekeo wa Sera Demokrasia na Mifumo yote tuliyonayo baada ya kupata Uhuru mwisho wake uwe ni ustawi, huduma bora na maendeleo ya watanzania. “Mnalo jukumu kubwa sana, katika kazi zenu kila mmoja anapofanya kazi zake aone anadhamana na Tanzania yake, amesema Waziri Mhagama.
Ameeleza kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo kazini muda wote, inapomaliza uchaguzi mmoja inajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine ikiwa ni pamoja na kuboresha Daftari la wapiga kura. Ametoa rai kwa wafanyakazi wa Tume ya taifa ya Uchaguzi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naye Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Katika taarifa yake amesema ujenzi wa majengo ya tume ya taifa ya uchaguzi unaendelea vizuri na unaelekea kukamilika, umebakiza shughuli ndogo ndogo zinazotakiwa kukamilika tarehe 31 Mwezi January 2022 tarehe . ujenzi wa jengo la utawala umekamilika kwa 99%, jengo la kuhifadhia vifaa limekamilika kwa 99% na jengo la kutangazia Matokeo ya Uchaguzi ujenzi umekamilika kwa 97%
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment