Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Kamandawa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa leo tarehe 29.12.2021 muda wa saa 02:00 asubuhi huko maeneo njiro block D JANEROSE D/O DEWASI umri miaka sitini na sita (66) mkazi wa njiro alikutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake huko maeneo ya njiro block D katika halmashauri ya jiji la Arusha huku mwili wake ukiwa na majeraha.
ACP MASEJO akitoa taarifaofisini kwake jion ya Leo amesema kuwa imebainika marehemu amepigwa na kitu chenye incha kali kwenye paji la uso upande wa kushoto kitendo kilichopelekea kupoteza uhai wake.
Ameeleza kuwa taarifa za awali zimebaini kuwa marehemu alikuwa akiishi nyumbani pamoja na mtumishi wa kazi za ndani aliyefahamika kwa jina moja la BONIFACE ambaye alianza kazi wiki moja iliyopita na muda mfupi kabla ya tukio hilo kugundulika alipotea kusiko julikana.
Amewambia waandishi kuwa Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea nauchunguzi wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kumsaka kijana huyo.
Kamanda Masejo ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha kuwa makini na kufuatilia mienendo ya wasaidizi wa kazi za ndani pindi wanapo wachukua ili waepusha madhara makubwa yanayoweza kujitokeza katika familia.Pia niwaombe wazazi kufuatilia mienendo ya ndugu na jamaa wanaoishi nao kama kuna viashiria vyovyote vya kutia mashaka mripoti katika vituo vya Polisi ili kuepusha madhara.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment