Na Khadija Kalili, Bagamoyo
Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir amewataka watanzania wote kuungana katika vita ya kujikinga na kirusi cha ugonjwa wa Uviko -19 ambacho kipo katika wimbi la nne duniani kote.
Ugonjwa huu upo ni hatari hivyo nawausia watanzania wote tuchukue tahadhari kubwa katika kujilinda na maambukizi ya Uviko-19.
Pia naomba nyote kulingana na juhudi za Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuchanja kwa wale wote ambao bado hawajachanja kwani chanjo hizi hazina madhara.
Mufti Zubeir alisema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya pili ya masomo yanayotokewa kwa nja ya mtandao na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye hafla iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Alisema kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wanapaswa kuzingatia suala la kutafuta elimu zote ya Dunia na Ahera na bila kujali umri kwa sababu elimu haina mwisho kwa mwanadamu.
Mahafali hayo ya pili ya kozi Uongozi na Utawala Bora TEHAMA yametajwa kuwa na wahitimu zaidi ya 1000 waliosoma kwa njia ya mtandao.
Aidha liwapongeza waumini wote ambao wamepata ujasiri wa kujiendekeza na mafunzo hayo huku akisisitiza kwa kusema kuwa mwamko waluounyesha waumini ni mzuri n umemfurahisha hivyo anatarajia idadi ya wahitimu mwakani itaongezeka na wameonyesha
waumini walivyokwenda sambamba na kauli mbiu isemayo 'Jitambue Wajibika wacha Mazoea'.
"Haya ni maneno matatu tu lakini ndiyo tunayoyaishi kutokana na ukiyanyumbulisha kwa mapana yake tunaishi nayo kidunia n akhera pia.
Alisema kuwa maendeleo yoyote ya kidunia na kidini ni suna hivyo hata kubadilika nako ni suna.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah alisema kuwa katika kuonyesha mfano wa kuuza kiwango cha elimu Wilayani hapa ametoa ufadhili wa vijana 50 ambao atawalipa ada ya masomo hayo na anatarajia katika mahali ya tatu watakuja kutoa ushuhuda wa elimu waliyoipata sanjari na kujiajiri.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment