MWENYEKITI HALMASHAURI YA CHALINZE MWINYIKONDO ASISITIZA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA MADARASA KABLA YA DESEMBA 28, 2021 | Tarimo Blog

Na Khadija Kalili, Chalinze

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo ametoa rai ya kusisitiza ufanyaji kazi kwa  bidii
 Ili kukamilisha miradi ya ugonjwa wa  Uviko- 19.

Mheshimiwa  Mwinyikondo ameyasema hayo  leo (Jana) na kuacha  kusherekea sikukuu ya  Chrismas na kufanya ziara ya ukaguzi wa madarasa ya  mradi wa Uviko- 19 ambapo aliambatana na jopo la Wataalam wa Halmashauri hiyo ya Chalinze  ili kukimbizana na muda uliobaki wa ukamilishaji wa majengo hayo.
Katika ziara hiyo Mhesgimjwa  Mwinyikondo amefanikiwa kutembelea jumla ya miradi mitano ya maendeleo iliyopo katika kata tofauti, ambazo ni pamoja na Shule ya Sekondari Kibindu, Shule Shikizi ya Komtonga, Shule ya Sekondari Kimange, Shule ya Sekondari Rupungwi na Shule ya Sekondari Changalikwa ambapo miradi  yote hiyo  ilipelekewa jumla Sh. Mil.320  kati ya Tsh Bil. 1.6 zilizopelekwa katika  Halimashauri hiyo kutekeleza jumla ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 80  yanajengwa.

Akizungumza katika ziara hiyo Mheshimiwa Mwinyikondo alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuisaidia Halmashauri hiyo ya Chalinze  katika kutatua tatizo la upungufu wa madarasa pia  amewataka wasimamizi na mafundi wa miradi hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuikamilisha kwa wakati ujenzi huo  na kufanikisha lengo kusudiwa ambalo ni kuchukuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema  ifikapo Januari 2022.

"Natoa wito wangu kwa wasimamizi wa miradi hii kwa maana ya Ofisi ya Mkurugenzi, Mhandisi wa Wilaya, Maafisa Elimu (Msingi na Sekondari) na Walimu Wakuu, Kamati za usimamizi na mafundi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha lengo la kukamilisha miradi hii mnamo tarehe 28.12.2022 linafikiwa’ alisema Mwenyekiti huyo .

Katika majumuisho ya ziara hiyo Mheshimiwa Mwinyikondo   aliwapongeza wataalam na wajumbe wote walioonyesha uzalendo na kuungana nae katika ziara hiyo japo ilikuwa ni sikukuu na kuwataka waendelee na.moyo  huo wa uzalendo.

Wakati huohuo  alimuagiza Afisa Mipango kuona namna ambavyo anaweza kupeleka fedha katika miradi kwa wakati hasa katika ujenzi wa vyoo kwenye shule zilizo bahatika kupata fedha za madarasa ya Uviko-19 ili kusaidia ukamilikaji wake kwa wakati.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2