WANANCHI WALIPWA ZAIDI MILIONI 200 IKUNGI XMASS | Tarimo Blog


Serikali imefanikisha malipo ya Shilingi Milioni 214 kwa wananchi 56 wa kata ya Mang’onyi ikiwa ni sehemu ya fidia ya Ardhi pamoja na makaburi 6 iliyochukuliwa na kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Shanta kwa ajili ya kuongeza uwekezaji wa mgodi

Akizungumza wakati akikabidhi hundi hizo kwa wananchi, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro amewashukuru wananchi kwa kumuamini na kumuachia jukumu la kusimamia zoezi la uthamini wa mwanzo mpaka kufikia kupatikana kwa malipo

Kwa upande wao wananchi ndugu wa familia 4 za Sawa wameishukuru serikali kwa kusimamia mwanzo wa zoezi mpaka kumalizika kwa wao kulipwa fedha zao ambazo zitawasaidia kipindi cha sikuu za Christmas na mwaka mpya pamoja na kugharamia shughuli za masomo kwa wanafunzi wao mwezi january

Hata hivyo katika utoaji wa hundi hizo familia mbili za Said Jumanne Hamis na mama Amina mohamed mghenyi hazikujitokeza kuchukua hundi zao zenye thamani ya milioni 41 kwa familia zote mbili

*Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi *




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2