Serikali imeokoa takribani Shilingi Bilion 4 baada ya kuamua kutekelezwa mradi wa Maji Kirando kwa Mfumo wa Force Akaunti kwa kutumia Taasisi zilizochini ya Wizara ya Maji ambazo ni Mamalaka ya Maji Sumbawanga na Wakala wa Maji Vijijini RUWASA.
Mradi huo ulitakiwa kutekelezwa kwa Bilion 7.7 na sasa utatekelezwa mpaka mwisho kwa Bilion 3.1
Mradi wa Maji Kirando ambao unatumia chanzo Cha Ziwa Tanganyika umekamilika kwa Wastani wa Asilimia 95 na umeanza kuwanufaisha Wananchi wa Vijiji 7 vya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa.Kabla ya mradi kuanza kutoa huduma ya Maji, Wananchi wa Kirando walikuwa wanatumia Maji ambayo si safi wala salama katika madimbwi ya Maji.
Mradi huo utawanufaisha Wakazi 74,341.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment