Wananchi hususani wakinamama kijiji cha Kisula jimbo la Nkasi Kusini wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Saluhu Hassan kwa kupata maji ikiwa walikua wakitembea umbali mrefu kutafuta maji hivo kupelekea ndoa zao kuwa mashakani.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amezindua Mradi wa Maji Kisula Wilayani Nkasi mkoani Rukwa uliyogharimu sh. 330,867,170 ambapo mradi huo utahudumia jumla ya wakazi 5027.
Aidha, Waziri Aweso ameahidi serikali ya awamu ya sita kutoa shilingi mil. 250 kwa ajili ya kumaliza changamoto ya Maji Kijiji cha Kasu jimbo la Nkasi kusini baada ya kupokea ombi la Mbunge Mhe.Vicent Mbogo aliezungumza kwa niaba ya wananchi.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amezindua Mradi wa Maji Kisula Wilayani Nkasi - Rukwa uliyogharimu sh. 330,867,170 mradi unahudumia wakazi 5027. Pia ameweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji Kirando na ameahidi wizara kutoa shilingi mil. 250 kwa ajili ya Kijiji cha Kasu kinachokabiliwa na changamoto kubwa ya Maji jimbo la Nkasi Kusini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment