UONGOZI MPYA TANZANIA GIRL GUIDES WAAHIDI MAKUBWA | Tarimo Blog

Kamishna Mkuu mpya wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA), Mary Richard akiapishwa na Kamishna wa TGGA, Wakili Victoria Mandari kushika wadhifa huo mara baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi katika mkutano huo.



Na Richard Mwaikenda

Mwanasheria Mary Richard amechaguliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA) katika mkutano Mkuu wa chama uliofanyika jijini Dar Dar es Salaam Desemba 13, 2021.


Mary na viongozi wengine wapya wa vijana wa TGGA, Mwenyekiti Irene Jeremiah na Katibu Amenciatha Makoko waliapishwa na Kamishna wa chama hicho, Wakili Victoria Mandari.Viongozi hao watahudumu katika nafasi hizo kwa miaka mitatu.

Kamishna Mkuu mpya, Mary amehidi kuendeleza mazuri yote ya uongozi uliopita kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa kufuata katiba ya chama hicho pamoja na kuwajengea uwezo vijana wa kike kujitambua na kufanya kazi kwa bidii kuliletea Taifa maendeleo na wao wenyewe.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni Kamishna Mkuu Msaidizi, Florentina Bernard na Makamu Mwenyekiti wa TGGA Taifa, Consolatha Shayo. Nafasi ya Mwenyekiti Taifa iko wazi baada ya kutopigiwa kura kutokana kutojitokeza wala kutoa udhuru katika mkutano huo.


Mwenyekiti mpya wa Vijana TGGA Taifa, Irene Jeremiah akila kiapo.

Katibu Mkuu wa Vijana Taifa wa TGGA, Amenciatha Makoko akila kiapo cha TGGA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Anna Maembe akiongoza Mkutano Mkuu wa TGGA uliofanya uchaguzi wa viongozi wapya.

Kamishna Mkuu wa TGGA, Mary Richard akitoa shukrani kwa wanachama kwa kumchagua kwa kura nyingi na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitumikia TGGA.

Mary Richard ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, akipiga kura wakati wa uchaguzi uliowaweka madarakani.

Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya Utendaji ya TGGA, Profesa Martha Qorro akipiga kura.

Kamishna Mkuu mstaafu wa TGGA, Symphorosa Hangi akipiga kura kuchagua uongozi mpya.


Mjumbe msataafu wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Zakhia Megji akichangia hoja wakati wa uchaguzi

Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Temeke, Komba akiuliza swali

Matokeo ya uchaguzi huo yakitangazwa

Katibu Mkuu wa TGGA, Wintapa Luila akitoa pongezi kwa uongozi mpya na shukrani kwa uongozi uliopita kwa ushirikiano walioutoa.

Wanachama wakiwa katika mkutano huo.












PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video viongozi wapya wakiapishwa na kuahidi kuchapa kazi kuifanya TGGA isonge mbele kimaendeleo, lakini pia Kamishna Mkuu mstaafu, Hangi akitoa neno......IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2