Raisa Said,Tanga
Benki ya NMB imeeleza nia yake ya kuendelea kushirikiana na serikali na wadau wa elimu ili kuinua ubora wa huduma za elimu mkoani Tanga.
Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mauzo wa NMB Kanda ya Kaskazini, Innocent Mwanga katika mahojiano baada ya ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Elimu Mkoa lililoandaliwa na Kundi la Whatsapp la SAUTI ya Tanga na kudhaminiwa na benki ya NMB.
Mwanga alisema kuwa Benki hiyo inafahamu kuwa elimu ni muhimu katika kuandaa rasilimali watu inayohitajika kufanya kazi katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Alisema benki hiyo ilikubali kufadhili kongamano hilo kama sehemu ya ari yake ya kuboresha ubora wa elimu na juhudi za mkoa za kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ufaulu katika mitihani ya mwisho ya darasa la saba umeshuka mfululizo kwa miaka miwili, ishara iliyowaamsha wadau wa elimu kuchukua hatua za kuboresha hali hiyo.
Mwanga alisema kuwa Benki imeshiriki katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, ununuzi wa madawati, ufadhili wa elimu ya wanafunzi wa shule za sekondari na uundaji wa bima ya elimu, Educare inayowawezesha wazazi kugharamia masomo ya watoto wao hata pale wanapokuwa wamefariki,
"Benki itaendelea kuwa sehemu ya juhudi za maendeleo ya elimu mkoa wa Tanga," alisema.
Naye Meneja wa NMB Mkoa wa Tanga, Elizabeth Chawinga alisema Benki hiyo itaendelea kudhamini kongamano la wadau wa elimu kila mwaka.
Akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Adam Malima alisema suala la kuinua ufaulu wa sekta ya mitihani unahitajika lakini akatahadharisha kuwa hilo halipaswi kuwa lengo pekee.
"Sio kuhusu namba tu, suala hapa linapaswa kuwa kuinua ubora wa elimu," alisema.
Malima alisema kuwa itakuwa haina maana kuwa katika nafasi za juu wakati ambapo wastani bado uko chini.
Alizungumzia haja ya kutatua changamoto zinazoathiri utendaji katika sekta ya elimu.
Aliwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya kufanya tathmini katika maeneo wanayosimamia ili kuelewa matatizo ya msingi yanayokwamisha maendeleo katika elimu.
"Unapaswa kufanya tathmini kujua kinachoendelea. Hatupaswi kuangalia namba. Tunapaswa kujua tatizo ni nini,” alisema.
Akizungumzia upungufu wa walimu aliwaagiza Wakurugenzi wa Wilaya kufanya tathmini na kuchukua hatua ili kuondoa tofauti za idadi ya walima kati ya maeneo ya mijini na vijijini.
Malima alisema kuwa ni jambo lisilokubalika kuona shule ya mijini zina walimu 38 huku shule ya vijijini ikiwa na walimu wanne.
Aidha alizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzisha ufuatiliaji wa shule ili kuhakikisha mambo yanakwenda kama ilivyopangwa.
Naye Mwenyekiti wa SAUTI ya Tanga, Mwantumu Mahiza alisema kitendo chao cha kuandaa kongamano hilo kilisababishwa na nia ya kutaka kuisaidia Tanga kuinua ubora wa elimu.
"Tumeangalia matokeo ya mihani kwa miaka miwili na tulifikiri tunapaswa kufanya kitu," alisema.
Meneja wa Bank ya NMB Tawi la Madaraka Elizabeth Chawinga akimkabidhi 'MIC'Afisa Mahusiano wa Bank hiyo Tawi la Madaraka.Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment